Serikali kuanzisha usafiri maalum kwa wanafunzi kupitia mwendokasi, Treni

February 4, 2026 4:57 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Usafiri huo unatajiwa kupunguza adha ya wanafunzi kuchelewa kurudi majumbani mwao.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imetangaza mpango mkakati wa kutenga mabasi ya wendokasi pamoja na mabehewa maalum ya treni kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi katika maeneo ya mijini, hatua inayotajwa kupunguza changamoto za usafiri kwa wanafunzi hao.

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa aliyekuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma leo Februari 4, 2026 amesema Serikali imechukua hatua hizo baada ya kusikiliza malalamiko ya wanafunzi kuhusu changamoto wanazokumbana nazo, ikiwemo kukataliwa kulipia nauli yao ya Sh200.

“Katika kuboresha usafiri wa wanafunzi mijini Serikali imeweka mipango na mikakati mbalimbali ikiwemo…kuanzisha huduma za mabasi maalum kwa ajili ya wanafunzi hususan katika nyakati za asubuhi na jioni ili kuhakikisha wanafunzi wanafika shule na kurejea majumbani kwao salama na kwa wakati,” amesema Prof Mbarawa.

Kwa miaka mingi wanafunzi hususani wa maeneo ya mijini kama jijini Dar es Salaam wamekuwa wakiteseka kupata huduma za usafiri hali inayowafanya aidha wachelewe kufika shuleni ama kufika nyumbani wakati wa kurudi.

Mbali na changamoto hizo, wanafunzi hao hulazimika kutumia muda mwingi barabarani au kutumia gharama kubwa kufika eneo la shuleni na wakati mwingine hujikuta katika hatari kubwa za kiusalama.

Aidha, Waziri Mbarawa ameielekeza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra), kupitia Mkurugenzi wake, Dk Habibu Suluo, kuimarisha udhibiti kwa madereva na makondakta na kuchukua hatua kali kwa watakaokiuka sheria.

Wizara pia imetoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kutoa taarifa na ushahidi wa vitendo vinavyokiuka sheria za usafiri wa ardhini kupitia namba za bure zilizowekwa ubavuni mwa kila daladala.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV