Santana: Filamu itakayokufundisha ubaya wa visasi

September 4, 2020 10:12 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Inahusu ndugu wawili waliopotezana utotoni baada ya wazazi kuuliwa kikatili.
  • Wanapobaini kuwa wazazi wao waliuwawa na nguli wa madawa ya kulevya anayeogopeka hata na mamlaka, wanaungana kulipiza kifo cha wazazi wao.
  • Mafunzo lukuki yanakungoja pindi utakapoitazama filamu hii kupitia Netflix.

Dar es Salaam. Utafanya nini ukimjua ndugu yako uliyetenganishwa naye tangu mkiwa watoto? Umepata jibu? Kaa nalo kisha linganisha kama linafanana na kilichofanywa na ndugu hawa.

Wakiwa watoto, wazazi wao wanauwawa na hapo ndipo wanapotengana.

Dunia inapoamua kuwakutanisha tena, ndugu hao wanaungana kulipa kisasi kwa muuaji aliye nyuma ya kifo cha wazazi wao.

Mambo yanazidi kupamba moto baada ya kumfahamu nguli wa madawa ya kulevya aliye nyuma ya kifo cha wazazi wao ambaye anaishi kana kwamba hakuna baya alilolifanya.


Zinazohusiana


Je, watafanikiwa kumuua ili kiu yao ya kisasi itimie? Usikose kutazama filamu ya Santana ambayo ni maalumu kwa watu wenye umri wa miaka 16 na zaidi kupitia mtandao wa Netfilx endapo umelipia kifurushi chako.

Pia, wikiendi yako inaweza kupambwa kwa kutembelea sehemu mbalimbali za kufurahisha macho na hata kujihusisha na shughuli za kijamii.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

Nukta TV

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Nukta TV