Sababu za Serikali kuziunganisha benki za TPB, TIB Corporate

June 1, 2020 1:01 pm · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link
  • Msajili wa hazina asema uamuzi huo umelenga kuboresha utendaji wa benki inazozimiliki ili kuwa na benki moja ya biashara ambayo ni imara.
  • Kwa hatua za awali TPB Bank PLC itachukua mali na madeni yote ya TIB Corporate.
  • TIB Corporate ni benki ya tatu ya umma kuunganishwa na TPB Bank PLC ndani ya miaka mitatu iliyopita.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imeziunganisha benki ya TPB Bank PLC na TIB Corporate ikibainisha kuwa uamuzi huo umelenga kuboresha utendaji wa benki inazozimiliki.

TIB Corporate ni benki ya tatu ya umma kuunganishwa na TPB Bank PLC ndani ya miaka mitatu iliyopita jambo ambalo linazidi kuiongezea nguvu benki ya TPB sokoni.

Msajili wa Hazina Athumani Mbuttuka ameeleza katika taarifa kwa umma kuwa uunganishaji wa benki hizo unaanza Jumatatu, Juni Mosi na kwamba kwa hatua za awali TPB Bank PLC itachukua mali na madeni yote ya TIB Corporate.

“Seikali imechukua uamuzi huu kwa lengo la kuboresha utendaji wa benki inazozimiliki ili kuwa na benki moja ya biashara ambayo ni imara,” amesema Mbuttuka.

“Aidha, muungano huu unalenga kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji, kimfumo, kimuundo na kitaswira ili benki hii iweze kuhimili ushindani wa kibiashara kwenye sekta ya fedha,” ameongeza bosi huyo.

Hata hivyo, Mbuttuka hakuweka bayana thamani ya uunganishaji wa benki hiyo wala nguvu ya kifedha ambayo TPB itakuwa nayo baada ya hatua hiyo.

Hii ni mara ya tatu Serikali inaziunganisha benki zake ndani ya miaka mitatu iliyopita. Mara ya kwanza iliziunganisha benki ya Twiga Bancorp na TPB PLC Mei 2018. Miezi mitatu baadaye iliziunganisha Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) na TPB Bank PLC Agosti 2018.


Zinazohusiana: 


Mbuttuka amesema wateja wote wa benki za TPB na TIB Corporate wataendelea kuhudumiwa kwenye matawi yao ya sasa hadi hapo wataKapoarifiwa vinginevyo.

“Serikali inawahakikishia wateja wa benki hizi mbili pamoja na umma kuwa huduma za kibenki hazitaathirika kwa vyovyote vile kutokana na mabadiliko haya,” amesema.

Uamuzi wa kuziunganisha benki hizo utafanya benki za biashara Tanzania kubakia 37 kutoka 38 zilizoripotiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mapema Januari 2020. 

Mbali na benki hizo za biashara, Tanzania ina benki sita za jamii, benki mbili za maendeleo na benki tano za huduma ndogo za kifedha (Microfinance banks).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
NISHATI

NISHATI

Nukta TV

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Nukta TV

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Nukta TV