Sababu za miguu kutoa harufu mbaya

October 12, 2020 12:28 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na uvaaji wa kiatu kimoja kwa muda mrefu na pia kuvalia kiatu ambacho kinabana.
  • unaweza kuepukana na adha ya harufu mbaya ya miguu kwa kuosha miguu yako mara kwa mara na kuikausha na kitambaa kisafi.
  • pia, unaweza kuwa na amani na harufi ya miguu yako kwa kuwa makini na soksi unazovalia.

Dar es Salaam. Kama wewe ni mmoja wa wahanga wa harufu mbaya ya miguu, huenda dondoo hizi zitakusaidia kubadilisha changammoto yako. 

Chanzo cha kutoa harufu kwenye miguu ni uwepo wa bakteria ambao wanasababishwa na jasho ambalo miguu hutoa inapokuwa kwenye joto.

Ajabu ni kuwa, unaweza kuepukana na changamoto hiyo kwa kubadilisha tabia mbalimbali za kila siku zinazohusisha miguu na viatu vyako.

Mathalan, tovuti ya afya ya Kids Health inaeleza kuwa, kuvaa viatu vinavyobana ni sababu mojawapo ya miguu kutoa harufu mbaya.

Miguu ikikosa hewa ya kutosha hutengeneza jasho kwenye kiatu na hivyo kuzalisha bakteria wanaoweza kuleta madhara kwenye miguu.

Njia mojawapo ya kutatua tatizo hilo ni kuiacha miguu ikae wazi au kuvaa viatu vya wazi.

Kwa dondoo zaidi, tazama video hii

Enable Notifications OK No thanks