Sababu lukuki za kwanini uangalie filamu ya “IT” wiki hii

September 6, 2019 12:25 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Imesheni visa vya kusisimua ambavyo vitakupa funzo la kuwa jasiri hata pale matatizo yanapokulemea. 
  • Filamu hiyo na ile ya sehemu ya kwanza zimeongozwa na Andrés Muschietti  ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 kwenye tasnia ya filamu. 
  • Utakutana mastaa wa filamu kama Jessica Chapstain akiwa na James McAvoy kuhakikisha Jokeri haondoki na roho nyingine tena kama alivyofanya miaka 27 iliyopita.

Dar es Salaam. Huenda kuanzia Jumatatu ya wiki hii hadi leo umekuwa kwenye majukumu ya hapa na pale ambayo yamekupa msongo wa mawazo na mengine kukuumiza nafsi. 

Kuyasahau hayo yote ama kupunguza ukubwa wake, unahitaji kufungua moyo wako ili upate burudani na kutuliza mawazo kwani kuwaza sana siyo salama kwa afya yako.

Nukta (www.nukta.co.tz) kwa yanayokuhusu  inakupa mapendekezo ya burudani ambazo zitakufaa katika mapumziko ya mwisho wa wiki. 

Kati ya burudani hizo, ni filamu ambazo zinaonyeshwa kwenye kumbi mbalimbali za sinema ikiwemo za Aura Mall na Mkuki House za Jijini  Dar es Salaam. Filamu itakayoonyeshwa wiki hii ni “IT” sehemu ya pili.


Zinazohusiana:


“IT” sehemu pili ina jipya?

Filamu hiyo na ile ya kwanza zimeongozwa na Andrés Muschietti (46) ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 kwenye tasnia ya filamu.

Ni filamu ya tatu yenye dhima za kutisha aliongoza Muschietti kuongoza ukiachilia ya IT sehemu ya kwanza na filamu ya Mama ya mwaka 2012. 

Usisahau vile “IT” sehemu ya kwanza ilisisimua mishipa ya hofu kwa watu wengi baada ya damu ya watoto wadogo kumwagika wakati walipokuwa wakimtafuta mdogo wa rafiki yao aliyepotea kwenye mazingira ya kutatanisha.

Katika sehemu ya pili, mazingira yanaanza kuwakumbusha kuwa kuna kazi ya miaka 27 iliyopita hawakuimaliza. Kazi hiyo ni kummaliza Jokeri ambaye aliwinda watoto wadogo na kuwauwa.

Ni filamu ya tatu yenye dhima za kutisha aliongoza Muschietti kuongoza ukiachilia ya IT sehemu ya kwanza na filamu ya Mama ya mwaka 2012. Picha|Mtandao. 

Tazama filamu hii kuona jinsi Jessica Chapstain (Dark Phoenix & The huntsman) akiwa na James McAvoy (Narnia & X-men) ambao wanashirikiana na marafiki zao kuhakikisha Jokeri huyo haondoki na roho nyingine tena kama alivyofanya miaka 27 iliyopita.

“IT” sehemu pili ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa, mpaka sasa kidokezo chake (teaser trailer) ambacho kimewekwa na chaneli ya Warner Bros. Pictures katika mtandao wa Youtube kimepata watazamaji wasiopungua milioni 43 mpaka mchana wa leo. 

Hata hivyo, kama ulikosa muda wa kutazama filamu za wiki iliyopita, bado una muda kwani filamu za Angel has fallen, Fast and Furious na Lion King bado zinaonyeshwa kwenye kumbi za sinema.

Naamini filamu hiyo ya “IT” itabadilisha kabisa mtazamo na kukurejeshea tabasamu usoni ili wiki inayofuata iwe yenye neema na ufanisi zaidi katika shughuli zako za uzalishaji mali.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV