Ruto avunja baraza la mawaziri Kenya

July 11, 2024 12:54 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema shughuli zote za Serikali zitaratibiwa na Katibu Mkuu wakati mchakato wa kupata baraza jipya ukiendelea.

Dar es Salaam. Rais wa Kenya William Ruto amevunja baraza la Mawaziri pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo Julai 11, 2024.

Ruto ametangaza kuwafuta kazi viongozi hao wakati akihutubia Taifa kupita televisheni ambapo amesema kuwa uamuzi huo umefanyika baada ya kufanya tathmini ya kina.

“Baada ya kutafakari, kusikiliza kwa makini kile watu wa Kenya walisema na baada ya tathmini ya kina ya utendaji wa Baraza langu la Mawaziri na mafanikio na changamoto zake, ninayo, kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa na Ibara ya 152(1) na 152(5)(b) ya Katiba Kifungu cha 12 cha Katiba. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, nimeamua kuwafuta kazi mara moja Makatibu wote wa Baraza la Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoka Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Kenya isipokuwa Waziri Mkuu na Waziri wa Masuala ya Nje na Diaspora,” alisema Rais Ruto.

Huenda huu ni muendelezo wa maboresho ya Serikali ya kiongozi hiyo kufuatia maandano ya vijana maarufu kama Gen Z yaliyofanyika kwa wiki kadhaa nchini humo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Nukta TV

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Nukta TV

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Nukta TV