Ruangwa watikisa matokeo darasa la saba mkoa wa Lindi.

November 19, 2018 6:28 pm · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Imeshika nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba kwa mkoa wa Lindi mwaka huu. 
  • Katika matokeo ya mwaka jana, Ruangwa ilishika nafasi ya tano kimkoa na kitaifa ilikuwa nafasi ya 141, ambapo kwa mwaka huu imepanda na kuwa nafasi ya kwanza kimkoa na kitaifa kuwa nafasi ya 84.
  • Walimu na wanafunzi waliofanya vizuri wapewa zawadi kama motisha ya kuwaongezea bidii ya kufundisha na kujifunza.

Dar es salaam. Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kwa kushika nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba kwa mkoa wa Lindi mwaka huu. 

Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ruangwa ametoa pongezi hizo jana  (Novemba 18, 2018) katika mkutano wa kuwapongeza walimu wa wilaya hiyo na baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka huu.

Katika matokeo ya mwaka jana, Ruangwa ilishika nafasi ya tano kimkoa na kitaifa ilikuwa nafasi ya 141, ambapo kwa mwaka huu imepanda na kuwa nafasi ya kwanza kimkoa na kitaifa kuwa nafasi ya 84.

Kufuatia matokeo hayo mazuri, Majaliwa ameta zawadi kwa kata tatu bora, shule 10 bora, walimu ambao wanafunzi wao wamepata daraja A katika masomo mbalimbali wanayofundisha pamoja na wanafunzi 10 bora katika halmashauri hiyo.

Miongoni mwa zawdi hizo ni pamoja na fedha taslimu, kompyuta kwaajili ya matumizi ya shule zilizofanya vizuri ikiwa ni kichocheo cha kuongeza bidii ili mwakani wapate matokeo mazuri zaidi.

Miongoni mwa zawadi hizo ni pamoja na fedha taslimu, kompyuta kwa ajili ya matumizi ya shule zilizofanya vizuri, ikiwa ni kichocheo cha kuongeza  bidii ili mwakani wapate matokeo mazuri zaidi.

Naye, mke wa Waziri Mkuu, mama Mary Majaliwa umeupongeza uongozi wa mkoa wa LIndi kwa mikakati waliyoiweka ya kuboresha elimu ambayo imesaidia kupatikana kwa matokeo hayo mazuri.

“Nawapongeza kwa sasa mimi kitaaluma ni mwalimu hivyo nafahamu ili mwanafunzi apate matokeo mazuri ni lazima mwalimu afanye juhudi kubwa zitakazomuwezesha mwanafunzi kufaulu masomo yake,” amesema mama Majaliwa.


Zinazohusiana: 


Kwa upande wake, Afisa Elimu Msingi wa wilaya ya Ruangwa, Mwalimu Selemani Mrope alisema kuanzia mwaka 2015 hadi 2017 hali ya ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba haikuwa nzuri kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya utoro.

Mwalimu Mrope alitaja sababu nyingine kuwa ni walimu kutowajibika ipasavyo, ufuatiliaji na usimamizi duni wa taaluma shuleni, ambapo viongozi wengi wa shule na kata walishindwa kusimamia ipasavyo majukumu yao na kuwaacha walimu wafanye kazi kwa mazoea.

“Wazazi wengi kukosa kuwajibika ipasavyo katika elimu ya watoto wao na kuona elimu haina maana kwao na kushindwa kuwahimiza watoto kwenda shule na kusababisha utoro huku wengine wakidiriki kuwashawishi watoto wao wafanye vibaya kwenye mitihani yao.”

Baada ya tathmini waliamua kuweka lengo la ufaulu wa asilimia 80 kwa mwaka huu na asilimia 90 mwaka 2019, hivyo walishirikisha wadau wote wakiwemo viongozi wa Serikali, walimu, wanafunzi, wazazi, viongozi wa dini, wazee maarufu na viogozi wa siasa. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
19 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
19 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
19 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV