Rejesha ardhi katika ubora wake ili kukuza uchumi:Thiaw

September 7, 2019 7:44 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Thiaw alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani kwa njia ya video kutoka New Delhi, India ambako anashiriki mkutano wa mkataba huo (COP14), unaofanyika tangu Septemba 2 hadi 13 ukiwa na kaulimbiu “kuwekeza katika ardhi, kufungua fursa”. Picha|Mtandao.


  • Katibu Mtendaji wa Mkataba wa Kuzuia Kuenea kwa Jangwa (UNCCD), Ibrahim Thiaw amesema  dunia sasa inatakiwa kuwekeza katika urejeshaji wa ardhi katika ubora wake.
  • Itasaidia kupunguza hatari za mabadiliko ya tabianchi  na hatari zinazoweza kuyumbisha uchumi.

Dar es Salaam. Katibu Mtendaji wa Mkataba wa Kuzuia Kuenea kwa Jangwa (UNCCD), Ibrahim Thiaw amesema  dunia sasa inatakiwa kuwekeza katika urejeshaji wa ardhi katika ubora kama njia mojawapo ya kuboresha ustawi wa maisha, kupunguza hatari za mabadiliko ya tabianchi  na hatari zinazoweza kuyumbisha uchumi.

 Thiaw alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani kwa njia ya video kutoka New Delhi, India ambako anashiriki mkutano wa mkataba huo (COP14), unaofanyika tangu Septemba 2 hadi 13 ukiwa na kaulimbiu “kuwekeza katika ardhi, kufungua fursa”.

“Ardhi inatupatia asilimia 99.7 ya nguvu tunazopata na maji tunayokunywa. Ardhi ni mchangiaji mkubwa katika uchumi wetu. Pia ina uhusiano na afya yetu. Dhoruba za mchanga na vumbi ni visababishi vya matatizo katika maeneo mengi ya dunia hususani yanayohusiana na magonjwa kama pumu,” amesema Thiaw.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa (UN), Thiaw amesema katika mwaka uliopita yaaani 2018, nchi 25 ziliingia katika dharura ya ukame; Zaidi ya nchi 70 zimeathirika na ukame na nchi za namna hiyo zinahangaika na uhaba wa chakula.


Zinazohusiana: 


Aidha, ameeleza kuwa kuna uhusiano kati ya amani na usalama, “hali katika eneo la Sahel (jangwa la Sahara) ni mchanganyiko wa sababu nyingi zikiwemo kushindania ardhi na maji. Watu wengi walioathirika wako barani Asia na eneo lililoathirika zaidi ni Afrika.”

Akijibu maswali ya Wanahabari, Thiaw amesema mkutano unaoendelea India unategemewa kukubaliana kuhusu maamuzi 30 katika mpango wa kuhakikisha malengo ya mwaka 2018 hadi 2030 yanafikiwa.

Pande zote zinazoshiriki zitapitisha makubaliano kuhusu udhibiti wa mmomonyoko wa udongo ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa UN wa mabadiliko ya tabianchi mnamo Septemba 23 mwaka huu ambao utaeleza kuwa uboreshaji wa ardhi ni sehemu moja ya suluhisho katika kupambana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV