Zana zitakazokusaidia kukuza biashara yako mtandaoni

July 1, 2020 1:14 pm · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Zana hizo za kidijitali zinakuwezesha kufuatilia mwenendo wa bidhaa na huduma unazotoa mtandaoni. 
  • Pia zinaweza kukusaidia kuimarisha mahusiano na wateja wako na kutafuta njia mbadala za kukuza soko. 

Dar es Salaam. Biashara yoyote ili ikue na kufanikiwa ni lazima ifanyiwe tathmini mara kwa mara. Tathmini inasaidia kufahamu jitihada na uwekezaji uliofanyika kama umeleta matokeo yaliyokusudiwa. 

Zipo za zana mbalimbali ambazo zinatumika kufuatilia na kuitathmini biashara yako, lakini leo tunakuletea zana za mtandaoni (Social media analytical tools) ambazo ni mahususi kwa biashara inayoratibu shughuli zake mtandaoni. 

Zana za tathmini katika mitandao ya kijamii ni muhimu kwa sababu zinasaidia katika kujua namna mitandao ya kijamii inachangia katika ukuaji wa biashara yako. 

Nukta (www.nukta.co.tz) inakuletea baadhi ya zana ambazo unaweza kuzitumia utendaji wa kampuni au biashara yako mtandaoni na kukusaidia kupata wateja wengi watakaotumia huduma na bidhaa zako:

Awario 

Ni moja ya zana hizo ambapo ina uwezo wa kukuonyesha watu wanaoitaja kampuni yako katika mitandao yao na kukuonyesha njia nzuri ya kuikuza na kuwafikia wa watu wengi zaidi. 

Zana hio pia ina uwezo wa kutathmini namna ambavyo maneno au misamiati ya kampuni yako imetumika nje ya kampuni na watu wengine. Unaweza kutumia zana hiyo kwa majaribio kwa siku 14 za majaribio, baada ya hapo utalazimika kulipa Dola za Marekani 29 (Sh66,666 ) ili kuendelea kuitumia.

Muonekano wa zana ya Awario. Picha|Mtandao.

Snaplytics 

Zana hiyo imetengenezwa maalum kwa ajili ya mtandao wa Snapchat na Instagram kwa ajili ya kutathmini maendeleo yake na kujua ni kwa namna gani jukwaa lako la mtandao husika linakua.

Kwa kutumia zana hii mtu ana uwezo wa kuona ni njia ipi inafaa zaidi katika kupromote platform yake kwa watu ili kuongeza idadi ya watu wanaotembelea akaunti yake.

Zana hiyo ya kulipia baada ya siku 14 za majaribio bila malipo.

Squarelovin 

Inatumiwa na watumiaji wa Instagram ili kupima maendeleo ya akaunti husika kwa kuzingatia muda, muingiliano (engagement) pamoja na mapendeleo ya watu (likes).

Inakuwezesha kuona na kukupa mapendekezo ya vitu vinavyoweza kuendana na huduma unayoitoa katika kampuni yako ili kupata watumiaji wengi zaidi katika akaunti yako ya Instagram. 

Ili kutumia zana hii haihitaji gharama zozote kwa maana ya fedha za kuiendesha.


Soma zaidi:


Rival IQ

Inampa uwezo mwendeshaji wa akaunti za biashara za mitandao ya Facebook, Twitter, Instagram kufahamu ni kwa jinsi gani wateja wake wanatembelea akaunti za kampuni husika na kuitumia kwa wakati anaopenda mwenyewe. 

Zana hii ina uhusiano na Google analytics na kumfanya mwendeshaji kujua wateja wanaotembelea akaunti yako na shughuli wanazofanya pindi wanapotembelea akaunti yako, pamoja na kuhakiki matangazo yanayokuja pindi unapofanyia kazi akaunti yako muda wowote.

RivalQ inavyoweza kukusaidia kukuza biashara yako mtandaoni. Picha|Mtandao.

Union metrics 

Ni zana nyingine inayomjulisha mwendeshaji wa akaunti za mitandao ya kijamii, post gani iliyotembelewa zaidi na ni kwa namna gani imetumika na watu wengine baada ya kutembelea ukurasa wako.

Key hole

Hii inatumika zaidi na Twitter na Instagram ambapo inasaidia kujua hatua iliyopigwa katika kutekeleza malengo ya kampuni mtandaoni na kukuonyesha maeneo yanayohitaji uwekezaji zaidi ili kuyafikia malengo husika siku zijazo.  

Hizo ni miongoni mwa zana zinazoweza kukusaidia katika kampuni yako ya kibiashara inayofanya kazi mtandaoni. Lakini uchaguzi wa zana inayokufaa uko katika uamuzi wako.

Enable Notifications OK No thanks