Watuhumiwa 13 wakamatwa kwa matukio ya uhalifu Mwanza

Mariam John 1034Hrs   Januari 15, 2024 Habari
  • Watuhumiwa kwa makosa ya mauaji, kughushi nyaraka na kusafirisha dawa za kulevya.

Mwanza. Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia  watuhumiwa 13 kwa kuhusika katika matukio matatu tofauti yakiwemo ya mauaji, kughushi nyaraka na kusafirisha dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mtafungwa aliyekuwa akizungumza na wanahabari Januari 15, 2024  jijini humo, amesema watuhumiwa hao waliokamatwa ni pamoja na  Selina Mchele (48) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Mwakilemwa na Maneno Mashauri (19) mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Lwenge iliyopo wilaya ya Sengerema.

Wengine ni Majaliwa Damas (22) Mganga wa tiba asili na  mkazi wa Masumbwe mkoani Geita, Ntingwa Kilimanjaro kwa jina maarufu Shetani(42) mkulima na mkazi wa kijiji cha Mbamba mkoani Geita na Emmanuel Damas (34) Mganga wa tiba asili na mkazi wa kijiji cha Burungwa mkoani Shinyanga.

"Watuhumiwa hao wanadaiwa kuhusika katika mauaji ya Sophia Maduka (61) na Mathias Lusesa (73) wote wakulima na wakazi wa Lwenge wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza,” amesema Mutafungwa. 

Baaadhi ya vitu vilivyokamatwa wakati wa doria ya polisi mkoani Mwanza.Picha|Mariam John

Kukithiri kwa mauaji hayo jijini Mwanza kutoa ishara ya kuhitajika nguvu ya ziada kwa Jeshi la polisi kuongeza doria na elimu ya kutosha kwa wananchi na waganga wa jadi kuachana na imani potofu zinazosababisha vifo.

Itakumbukwa kuwa Disemba 2023 Kamanda Mutafungwa alifanya kikao na waganga wa jadi zaidi ya 500 mkoani humo akiwataka kushirikiana na Jeshi la Polisi kuzuia matukio ya mauaji 

Aidha, Mutafungwa ameeleza kuwa wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu sugu wa usafirishaji na uuzaji wa dawa za kulevya ambao wamekuwa wakisafirisha kupitia barabara ya Mwanza – Musoma kwa kutumia magari binafsi.

Watuhumiwa hao ni pamoja na Peter Charles kwa jina maarufu Peter Mirungi (50), Said Abdallah (27) na Emenn Gamariel kwa jina maarufu Munuo (30) wakazi wa Igoma Wilaya ya Nyamagana.


Soma zaidi:Nchimbi Katibu Mkuu mpya CCM


"Baada ya mahojiano ilibainika kuwa gari namba T.406 EAM Toyota Alphard lilikuwa likisindikiza gari namba T. 481 AJZ Toyota Surf lililokuwa limebeba shehena ya Mirungi ili lisikamatwe,” ameeleza Mutafungwa.

Jeshi hilo pia limemkamata mtuhumiwa sugu wa kughushi nyaraka anayejulikana kwa jina la Majaliwa Philipo Mwaikambo (34)  kwa kosa la kughushi nyaraka za watumishi wa Serikali kwa ajili ya kupata mikopo katika taasisi mbalimbali za kifedha.

Mtuhumiwa huyo alishiiriikiana na wenzake wanne kughushi nyaraka walizotumia kusitisha marejesho ya mikopo waliyopa Serikalini lenngo likiwakujipatia fedha kinyumena sheria.

Watuhumiwa wote wamehojiwa kwa kina na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Related Post