Watumia miaka mitano kuchimba sanamu ya miaka 3000 Misri
Farao sio jina geni katika simulizi za vitabu vyetu vitukufu vya Biblia na Quran kwa mikasa yake, visa na masaibu yalimpata pale alipokutana na adhabu za mwenyezi Mungu. Farao ni jina lilokuwa linatumika kama mfalme wa Misri.
Inasemekana Waisrael walipokuwa Misri walimjengea mfalme huyo Ramses miji ya Pithomu na Ramesesi. Miaka tarkibani 3000 tangu enzi za ufalme wake, hivi karibuni katika mji wa Matarlya Kaskazini mwa jiji la Cairo nchini Misri imeripotiwa kuwa kugundulika kwa sanamu la mfalme huyo. Wataalamu wa mambo ya kale kutoka Misri na Ujerumani wanasema sanamu hiyo iliyopatikana chini ya ardhi inafanana kabisa na ya Farao Ramses wa pili aliyetawala kwa miaka 66 kutoka 1213 BC hadi 1279BC.
Ingawa hakukuwa na alama yoyote ya kumwonyesha kuwa ni yeye, lakini wataalamu hao wamesema kugundulika karibu na sinagogi inatoa picha ya kuwa sanamu hiyo ni ya Farao Ramesi wa pili.
Wanahistoria wanamueleza Farao Ramesi wa pili kama kiongozi wa pili aliyetawala muda mrefu katika himaya ya kifamle vilivile anasifika kwa ujemedari wake. Farao huyo aliyetawala wakati wa Misri ya kale kabla ya ujio wa kristu kwa miaka ipatayo 66, historia inaeleza zaidi kuwa katika kipindi cha utawala wake aliweza kuitawala Nubia kama inavyojulikana sasa Sudani na Syria.
Tukio hilo la aina yake liliokea Machi 9, 2017 huku ikiwa imeripotiwa kuwa utafiti huo ulianza tangu mwaka 2012.
Ukubwa wa sanamu hiyo ilifanya wanasanyansi hao wa mambo ya kale kutumia greda kuichimba kutoka ardhini ingawa jambo hilo lilipingwa na watu wengi. Kitendo cha wananchi wengi kupinga sanamu hiyo kufukuliwa na tingatinga kulimlazimu Waziri wa nchi hiyo Khaled al-Anani kufafanua kuwa walilazimika kufanya hivyo kutokana na uzito mkubwa uliopo kwenye kichwa cha sanamu hiyo.
“Ipo wazi kuwa uzito wa kichwa cha sanamu hiyo ndio sababu ya kutumia greda lakini haikuharibiwa wakati wa uchimbaji.”amesema waziri Khaled al-Anani,.
Akifafanua zaidi amesema wataalamu wa mambo ya kale bado wanafanya kazi ya kuondoa sehemu kubwa ya hiyo sanamu ilipo aridhini. Farao huyo aliyejulikana pia kama Ramses.
Kupitia ugunduzi huo pia watalamu hao wa mambo ya kale wamegundua inchi 31 ya sanamu ya mjukuu wa mfalme huyo anayejulikna kama Site II.
Profesa Dietrich Raue kutoka katika Chuo Kikuu cha Leipzig cha Ujerumani, aliyongoza timu ya wataalamu wa mambo ya kale kutoka nchini humo katika uchimbaji huo, mesema kazi kubwa waliyoianza mwaka 2012 inafika mwisho.
‘’Ili kuwa ni eneo ambalo tayari lilikuwa limeshafanyiwa utafiti na tulidhani hakuna kitu lakini huu ni mshangao kwetu,” amesema Prof Raue.
Wanataaluma hao wa mambo ya kale wanakadiria kuwa sanamu hiyo ya Farao Ramses wa pili ikisimamishwa ina urefu wa takribani futi 30 kutokea ardhini.
Sehemu ya sanamu hiyo ambayo ni kichwa na kiwiliwili inatarajiwa kupelekwa kwenye makumbusho ya heshima ya Misri (Grand Egyptian Museum Kiingereza) yaliyopo Giza yanayotarajiwa kufunguliwa mwakani.