Wasichana, wavulana 10 bora matokeo kidato cha nne 2020
- Wasichana wanaongozwa na Justina Pious huku Wavulana wakiongoozwa na Paul Luziga.
- Wasichana wanne walioshikilia nafasi za juu wanatokea Shule ya Sekondari Canossa.
- Upande wa wavulana, Shule za Sekondari za Mzumbe na Marian Boys ndizo zimeingiza wanafunzi wengi zaidi.
Dar es Salaam. Leo ni siku ambayo watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2020, wanavuna walichopanda baada ya baada ya Baraza la Mitihani la Tanzania (Nekta) kutangaza matokeo ya mtihani huo.
Necta imeeleza kuwa katika mtihani huo watahiniwa wa shule 373,958 wamefaulu mtihani kati ya wanafunzi 434,654 waliofanya mtihani huo Novemba mwaka jana ikiwa ni sawa na asilimia 85.84 ya watahiniwa wote.
Ufaulu huo, kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, ni sawa ongezeko la asilimia 5.19 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2019. Mwaka juzi asilimia 80.65 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo.
Katika matokeo hayo, Necta pia imetoa orodha ya wavualana na wasichana waliofanya vizuri katika mtihani huo.
Orodha ya wasichana 10 bora imeongozwa na shule ya Canossa iliyopo jijini Dar es Salaam ambayo imefanikiwa kuingiza wasichana wanne walioshikilia nafasi nne za kwanza wakiongozwa na Justina Gerald akifuatiwa na Layla Atokwete, Lunargrace Celestine na Catherine Mphumuhila aliyeshika nafasi ya nne.
Nafasi ya tano imeenda kwa Happyness Matata kutoka shule ya Musabe Girls ya jijini Mwanza huku Debora Mwenda wa St Francis Girls ya jijini Mbeya akishika nafasi ya sita.
Mwanafunzi bora wa kike katika nafasi ya saba ni Rose Kaale wa Precious Blood (Arusha) anayefuatiwa na Wendo Manyelezi kutoka Marian Girls ya mkoani Pwani katika nafasi ya nane.
Nafsi ya tisa imeshikiliwa na Bellin Mungunasi wa St Francis huku orodha hiyo ikifungwa na Nancy Mung’azo wa St Francis.
Justina mbaye amekua msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo hayo ambaye ana ndoto ya kuwa mhandisi wa gesi na mafuta amesema siri ya ushindi wake ni kufanya mambo yote kwa kiasi. Picha| Justina Pious.
Msichana wa kwanza kitaifa azungumza
Akiongea na Nukta, Justina mbaye amekua msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo hayo ambaye ana ndoto ya kuwa mhandisi wa gesi na mafuta amesema siri ya ushindi wake ni kufanya mambo yote kwa kiasi.
“Ninasoma kwa kiasi, napumzika kwa kiasi, ninaburudika kwa kiasi lakini kubwa zaidi, ninamtegemea Mungu,” amesema binti huyo ambaye kwa mujibu wa baba yake, anamtazamia
Binti huyo amesema ana furaha isiyo na kifani kwa sababu hakutegemea kuwa mwanafunzi bora wa kike, licha alikuwa akifanya vizuri katika masomo yake shuleni.
Licha ya Cannosa kutoa mwanafunzi bora wa kwanza, pia imefanikiwa kushika nafasi ya tatu kitaifa ikiwa chini ya St. Francis ya Mbeya na Ilboru ya mkoani Arusha.
Baba wa Justina, Gerald Pious amesema anaamini kilichomsaidia zaidi binti yake kufanya vizuri ni unyenyekevu wake kwa Mungu na tabia yake ya kujisomea zaidi vitabu vya mtaala na vitabu vingine vya kumjenga kifikra.
Naye baba mzazi wa Layla aliyeshika nafasi ya pili kitaifa kwa upande wa wasichana, Khalfan Atokwete amesema, hakutarajia mtoto wake kuwa na matokeo hayo hasa baada ya ugonjwa wa Corona kutangazwa nchini na kusababisha wanafunzi kurudi nyumbani.
“Nilikuwa na wasiwasi sana lakini juhudi zake zimemsaidia. Layla siyo wa kusukumwa inapokuja katika kujisomea. Anajua majukumu yake na anayatekeleza vizuri,” amesema baba Layla ambaye mtoto wake alikuwa “kipanga” ama almaarufu kama “TO” wa kidato cha pili mwaka 2018.
Paul Luziga amebainisha kumtegemea Mungu na kusoma kwa juhudi ndiyo siri ya mafanikio yake. Picha| Paul Luziga.
Wavulana 10 bora kidato cha nne
Kwa upande wa wanafunzi bora wa kiume katika matokeo hayo, orodha hiyo imeongozwa na Paul Luziga ambaye ni mwanafunzi bora wa jumla kitaifa kutoka Shule ya sekondari ya Pandahill ya mkoani Mbeya.
Nfasi ya pili inashikiliwa na Timothy Segu kutoka Shule ya Sekondari ya Mzumbe ya mkoani Morogoro.
Nafasi ya tatu inashikiliwa na Isaya Rukamya wa Feza Boys (Dar es Salaam) akifuatiwa na Ashrafu Ally wa lboru (Arusha). Namba tano imeshikiliwa na Samson Mwakabage wa shule ya Sekondari Jude (Arusha) na namba sita ikiwa kwa Derick Mushi wa Ilboru wa mkoani humo.
Nafasi ya saba imeenda kwa Innocent Joseph wa Mzumbe, nafasi ya nane imeenda kwa John Maro wa Msolwa (Morogoro), nafasi ya tisa imeenda kwa Baraka Nyigo wa Marian Boys ya mkoani Pwani na nafasi ya 10 imebaki shule hiyo hiyo ikishikiliwa na John Rugemalila.
Kwa matokeo hayo, mikoa ya Arusha na Morogoro ndiyo imeingiza shule nyingi kwenye orodha hiyo ya 10 bora ya wavulana baada ya kutoa tatu kila moja huku Pwani ikiingiza shule mbili.
Soma zaidi:
- Huyu ndiye mwanafunzi bora kidato cha nne mwaka 2020
- Shule 10 bora kidato cha nne mwaka 2020 hizi hapa
- Bagamoyo kinara matokeo kidato cha nne mwaka 2020
Akiongea na Nukta (www.nukta.co.tz), Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mzumbe ambayo imeingiza wanafunzi wawili katika orodha hiyo, Wenceslaus Lundamasasi amesema mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi za walimu na wanafunzi lakini kubwa zaidi “ni Mungu tu”.
Lundamasasi ameeleza kuwa, malengo ya shule hiyo ni kuwa bora kitaifa katika matokeo ya mwakani na ukarababti wa shule hiyo ya Serikali umefanya wanafunzi kuwa na mazingira mazuri ya kujisomea na hivyo kuchagiza mafanikio ya elimu ya wanafunzi wa shule hiyo.
“Lengo letu ni kufikia kileleni. Tunaamini mwakani tutakuwa shule bora katika matokeo ya kidato cha nne,” amesema.
Shule hiyo kongwe ya Serikali imeshika nafasi ya
Hii ndiyo orodha ya jumla ya wanafunzi 10 bora kitaifa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2020 inayojumuisha wavulana na wasichana.