The Informer: Filamu ya mwisho kuitazama Januari 2020

January 24, 2020 8:05 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Simu hiyo inamtaka Koslow kufanya kazi ya mwisho ili awe huru kabisa na asisikie polisi wakimtafuta tena. Picha| Dailymotion.


  • Imejaa visa vya uhalifu, usaliti na mapenzi.
  • Inawakusanya mastaa wengi akiwemo Rappa Common.
  • Imegharimu kiasi cha zaidi ya Sh5 bilioni.

Dar es Salaam. Licha ya kubaki na Januari kwa muda mrefu, mwezi huo pendwa unaelekea mwishoni sasa.

Na hiyo ndiyo sababu kubwa ya kuhakikisha kuwa hauikosi filamu ambayo inasindikiza mwisho wa mwezi huu kabla hujaingia mwingine. Inafurahisha siyo?

Chagua kuanza wikiendi hii kwa furaha na bashasha kwa kutoka na marafiki au yule umpendaye na kwenda kutazama filamu ya kivita, “The Informer” katika kumbi za sinema Tanzania zikiwemo za Century Cinemax. 

Filamu hiyo ambayo imeongozwa na Andrea Di Stefano ambaye ameongoza filamu nyingi zikiwemo “Life of Pi” na “Escobar Paradise Lost”, inasimulia kisa cha kihalifu kinachohusisha maafisa upelelezi, usaliti, rushwa na hali ya njiapanda.

Unahisi maisha yako ni magumu? Chini ya donge la Sh5.07 bilioni lililowezesha filamu hii, Pete Koslow (Joel Kinnaman) ambaye ni mhalifu aliyebadilika na hapo awali askari wa kitengo maalumu analazimika kuicha familia yake ambayo inaonekana kuwa na furaha baada ya mlio wa simu.

Ndiyo! Simu hiyo inamtaka Koslow kufanya kazi ya mwisho ili awe huru kabisa na asisikie polisi wakimtafuta tena.

Hata hivyo, kazi hiyo kwa Koslow inazidi kuwa ngumu pale afisa mpelelezi anapokufa mbele yake. Jambo hilo linafanya vyombo vya dola kuingilia kati kutafuta ukweli wa chanzo cha kifo cha mtumishi huyo wa umma.

Kama ni wimbo, basi hapo ndipo korasi inaanza kwani upelelezi anaoufanya Koslow, haufahamiki na vyombo vya dola bali ni mchongo wa wadau wawili ambao ni  Wilcox (Rosamund Pike) na mwenzake  Montgomery (Clive Owen).

Pale Mpelelezi Grens (Common) kutoka mamlaka kuu anaposhikilia kesi hiyo kuchunguza ukweli juu ya kifo cha rafiki yake, Montgomery na Wilcox wanamgeuka Koslow na kuamua kumuangamiza yeye na pengine familia yake.


Zinazohusiana


Rushwa itamponza nani? Ukweli ni upi? Na maswali mengine yote uliyonayo yanaweza kujibika kwa kutoa Sh10,000 na kuitazama filamu hii kwenye kumbi za filamu za Century Cinemax zilizopo kwenye takriban kila duka kubwa “Mall” jijini Dar es Salaam.

Na hakika utaifurahia “The Informer” lakini kama hiyo siyo fungu lako pendwa, “Bad Boys For Life”, “Dr Dolidle”, “Jumanji” na hata “Spies in Disguise” bado zipo kwenye kumbi hizi kwe bei hiyo hiyo.

Wiki ijayo kuna nini? Kaa chonjo.

Enable Notifications OK No thanks