Safari ya mwisho ya Maalim Seif kuhitimishwa leo Zanzibar

February 18, 2021 2:31 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link


  • Mwili wa Maalim Seif unatarajiwa kuzikwa katika kijiji cha Matembwe kisiwani Pemba. 
  • Kabla ya mazishi, mwili wake utafanyiwa sala tatu jijini Dar es Salaam, Unguja na Pemba. 
  • Maalim Seif atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi wa Taifa la Tanzania.

Dar es Salaam. Mwili wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad unatarajia kupumzishwa leo Februari 18, 2021 katika kijiji cha Mtambwe kisiwani Pemba, ikiwa ni siku moja tangu kutangazwa kwa kifo chake.

Maalim Seif aliyezaliwa mwaka 1949 amefariki dunia jana Februari 17 saa 5:00 asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaan alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, mwili wa Maalim Seif umesafirishwa kuelekea Unguja, Zanzibar baada ya sala ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika msikiti wa Maamur jijini Dar es Salaam.

Mwili wa kiongozi huyo wa juu Zanzibar utakapowasili Unguja utapelekwa  katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa ajili sala ya marehemu ambayo itaongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Swaleh Omar Kabi

Baada ya sala hiyo itakayofanyika majira ya saa 5:00 asubuhi, mwili pamoja na wafiwa wataelekea kisiwani Pemba ambako ndiko chimbuko la Maalim Seif.

Huko nako atafanyiwa sala katika uwanja wa Gombani ambapo sala hiyo itaongoza na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Shehe Khalid Ali Mfaume. 

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa baada ya sala hiyo, mwili wa Maalim Seif utasafirishwa kuelekea kijiji cha Mtambwe ambapo mwili utafanyiwa sala kabla ya kuzikwa saa 10:00 jioni.


Soma zaidi:


Hiyo ndiyo itakuwa safari ya mwisho ya miaka 78 ya kuishi kwa kiongozi huyo mashuhuri Zanzibar na Tanzania.

Enzi za uhai wake, Maalim Seif aliwajibika kama Mwenyekiti wa Chama Cha ACT-Wazalendo, mwanachama wa Chama Cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amewahi kushika nyadhfa mbalimbali za kiuongozi ikiwemo Waziri Kiongozi wa Zanzibar mwaka 1984 hadi 1988.

Pia, mwaka 2010 hadi 2015, Maalim Seif ilitumika kama Makamu wa kwanza wa Rais Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK).

Endelea kufuatilia Nukta Habari kwa ukaribu kupata taarifa zaidi kuhusu msiba huo wa kitaifa.

Enable Notifications OK No thanks