Namna ya kutumia TinEye kukabiliana na picha za uzushi

June 1, 2020 2:43 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Unatakiwa kuzifuata  hatua zote nne ili uweze kufanikiwa kujua kama picha hiyo ilishawi chapishwa tena ama la.

Dar es Salaam.Habari nyingi za ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) zimekuwa zikisambaa kwa mtindo wa habari picha kwenye mitandao ya kijamii hususan kwenye makundi ya WhatsApp ambapo kwa sasa imekuwa ni chanzo kikubwa cha kutoa habari za uzushi.

Lakini sasa kwa kutumia nyezo za kidijitali  kama “TinEye” unaweza kubaini ukweli wa picha hiyo hususan muda wa kuchapishwa mtandao na chanzo chake cha awali.

TinEye huweza kumsaidia mtu yoyote akiwemo mwandishi wa habari katika kutafuta ukweli kuhusu picha husika na kujua picha ilichapishwa kwa mara ya kwanza lini na tovuti au mtandao gani ili kupambana na nia ovu.

Hatua ya kwanza

Unapopata picha unayoitilia shaka kuhusu ukweli wake hatua ya kwanza  nikutafuta nyezo hiyo ya kijigitali katika kitafutio ‘’browser “ chako  unachotumia  kama ni mtandao wa Google au mwingine kwa kuandika neno “tineye.com”

Kisha itatatokea majibu kwa jina la “TinEye Reverse Image Search” utatakiwa kubonyeza hapo kwenye maneno hayo ambapo utapelekwa kwenye ukurasa wa nyenzo hiyo moja kwa moja.

Hatua ya pili

Hatua ya pili baada ya kufika katika ukurusa huo utakutana na maneno makubwa yanayosomeka “ Reverse Image Search” na chini yake kuna maneno mengine yanayosomeka tafuta picha ilipo kwenye mtandao (Search by image and find where that image appears online).

Katika maneno hayo ndiyo sehemu ya kutafutia picha ilipo ambapo  katika mkono wako wa kushoto utaona alama ya kuchapishia picha cha mshale unaongalia juu pia utaona sehemu ya kutafutia picha pembeni yake.

Hatua ya tatu

Sasa mtumiaji katika hatua ya tatu atatakiwa kuweka picha hiyo anayoitilia shaka kwa kutumia namna mbili ya kwanza kwa kupakia picha hiyo (upload image ) kutoka mtandaoni au kwenye kompyuta yake kwa kubonyenza kimshale kinachoangalia juu kilichopo mkono wako wa kushoto.

Namna ya pili kwa kutumia kiunganishi (Paste image URL) kutoka kwenye picha hiyo.

Hatua ya nne

Mara baada ya kupandisha picha katika hatua hiyo ya nne utaweza kuiona TinEye imeleta majibu  na hii ni endapo tu picha hiyo unayotilia shaka imeshawahi kuchapishwa kokote pale mtandaoni. Lakini kama haijawahi kuchapishwa kwenye mtandao haitaleta majibu yoyote.

Jambo zuri kuhusu TinEye ni kwamba utaweza kutumia pia kwa njia ya simu yako ya mkononi lakini utatakiwa kufuata hatua hizo zote zilizo elezwa hapo juu.

Enable Notifications OK No thanks