Mwanzo, mwisho wa Robert Mugabe

September 6, 2019 10:13 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Amefariki akiwa na umri wa miaka 95 
  • Alikuwa na uwezo mkubwa darasani na amefariki akiwa na shahada saba. 
  • Aliondolewa madarakani mwaka 2017 baada ya kutawala nchi kwa miaka 37. 
  • Atakumbukwa zaidi kwa mchango wake wa kupigania ukombozi wa bara la Afrika. 

Dar es Salaam. Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa nchini Singapore ambako alikuwa anapatiwa matibabu kwa muda mrefu sasa. 

Rais wa sasa wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa amethibitisha kutokea kwa kifo cha Mugabe aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95 kupitia ukurasa wake waTwitter. 

Alikuwa kiongozi wa Zimbabwe toka 1980 mpaka 2017 na ni baba wa Taifa hilo kwa sababu aliongoza mapambano ya kudai uhuru hadi nchi hiyo ilipotoka katika mikono ya wakoloni wa Kiengereza. 

Unaijua safari yake tangu akiwa mdogo hadi anafariki? www.nukta.co.tz inakuchambulia maisha ya Mugabe katika familia, elimu na uongozi.

Maisha yake.

Mugabe alizaliwa Februari 21, 1924 nchini Zimbabwe ambayo awali ilikuwa inaitwa “Southern Rhodesia” enzi za wakoloni. 

Rais huyo aliyetambulika kama mtu mwenye uwezo mkubwa darasani alikuwa mtoto kati ya watoto sita kutoka kwa wazazi wake Gabriel na Bona Mugabe. 

Mugabe alioa wake wawili, wa kwanza akiwa Sarah Heyfron ambaye alizaa nae mtoto mmoja aliyeitwa Michael Nhamodzenyika Mugabe na baada ya kifo cha mke wake mwaka 1992, alimuoa msaidizi wake Grace Marufu  1996 aliyezaa naye watoto watatu; Bona Mugabe, Chatunga Bellarmine Mugabe, Robert Peter Mugabe Jr.


Zinazohusiana:


Safari ya kuitafuta elimu 

Mugabe alibahatika kuwa na kiwango kizuri cha elimu katika shule ya Local Jesuit moja ya shule za kimisionari, iliyomfundisha Mugabe namna ambavyo watu wanatakiwa kupata elimu na kiwango wanachotakiwa kufikia katika safari ya kitaaluma.

Baada ya kumaliza elimu ya awali Mugabe aliendelea kujisomea mwenyewe bila kwenda shule na kuhamia kuwa mwalimu katika shule za kimisionari huko Southern Rodesia ambayo kwa sasa inajulikana kama Zimbabwe.

Mugabe aliendelea na Elimu yake ya juu katika chuo kikuu cha Fort Hare, Afrika Kusini na kupata shahada ya kwanza katika somo la historia na kiingereza mwaka 1951 na baadaye kurudi kwao na kuwa mwalimu.

Kwa jumla, Mugabe ana shahada saba na alisomea shahada zake nyingine kupitia mtandao akiwa gerezani hasa katika taaluma ya elimu, sayansi, sheria na usimamizi.

Rais Mugabe akiwa na mke wake Grace. Alipendelea kuwa nadhifu hasa kwa mavazi ya vitengete. Picha|Mtandao. 

Safari yake ya kisiasa.

Mwaka 1960 Mugabe alirudi nchini kwao kutoka Ghana, kwa jili ya likizo, katika kukaa kwake aligundua vurugu nyingi zilizokua zikiendelea kwao huko Southern Rodesia 

Mugabe alikua mwanzilishi wa chama cha The Zimbabwe African National Union – Patriotic Front (ZANU–PF) ambacho kinatawala mpaka leo chini ya Rais Mnangagwa.

Mugabe alianza kwa Waziri Mkuu wa Zimbabwe mara baada ya utawala wa wazungu mwaka 198 ambapo Desemba 30, 1987 alichukua madaraka ya kuwa rais wa nchi hiyo.

Mugabe alikaa kwenye kiti cha urais tangu mwaka 1987 hadi alipoondolewa kwa nguvu katika kiti cha urais mwaka 2017, akiwa na miaka 93. 

Atakumbukwa kwa mengi hasa mchango alioutoa katika ukombozi wa bara la Afrika na kupinga dhuluma zilizokuwa zinafanywa na mabepari kwa Waafrika.

Enable Notifications OK No thanks