Msitu wa Magoroto ni zaidi pepo ya utalii Tanzania

April 20, 2021 9:51 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Umesheheni mandhari nzuri na yenye kuvutia kwa watalii wa ndani.
  • Imejificha Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga.

Dar es Salaam. Wapo ambao tafsiri ya mapumziko ni kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii ikiwa ni sehemu ya kubadilisha mazingira waliyoyazoea na kujifunza vitu vipya.

Basi kama wewe ni miongoni mwa watu wanaopenda utalii, sehemu sahihi ya kwenda kabla ya kuisha kwa mwaka huu ni katika msitu wa Magoroto uliopo Wilaya ya Muheza,  kilomita 37 toka katika Jijini la Tanga.

Msitu huo wenye ukubwa wa ekari 591 na ziwa la maji masafi, ulifunguliwa mwaka 1896 na Watalawa wa Kijerumani kama shamba la kwanza la kibiashara Afrika Mashariki.  

Kwa mara ya kwanza shamba hilo lililima zao la mpira baada ya kushindwa kulima kahawa na chai na baadaye kulimwa michikichi mwaka 1921. Hii ni stori siku nyingine.

Hivi karibuni timu ya Nukta Habari (www.nukta.co.tz) na washirika wake K15 Photos tulifanya ziara katika msitu huo ili kujionea uumbaji wa asili wa Mungu. Uzuri tulioufaidi hatukutaka tubaki nao lakini tumekuletea na wewe msomaji wetu.

Tazama picha hizi kujionea mandhari ya eneo hilo ambalo ukifika unaweza kufanya shughuli mbalimbali za utalii ikiwemo kupanda milima na kuogelea kwenye ziwa lenye maji yanayotiririka toka nyanda za juu za milima yenye maua na majani ya kupendeza.

Ndege wazuri wenye milio ya kila aina watakukaribisha katika msitu huo ili kujionea mandhari nzuri na ya kipekee. Picha| K15 Photos.

Fursa ya kutembea, kupanda milima na kuendesha baiskeli nayo inakusubiri ili kujionea uzuri uliopo katika msitu huo ambao unatajwa kama pepo ya aina yake Tanzania. Picha| K15 Photos.

Kama ni maji basi utayapa yaliyotulia yanayobubujika kutoka kwenye miamba na mlima Usambara ambao unazunguka msituo huo. Picha| K15 Photos.

Unahitaji muda wa kukaa pekee yako na kutafakari kuhusu maisha na mstakabali wa maisha yako. Picha| K15Photos.

Kwa wenzangu na mimi ambao wanapenda kupiga kambi pembeni ya ziwa, basi Magoroto ni sehemu sahihi. Picha| K15 Photos.

Ndani ya mtumbwi ukiwa juu ya maji tulivu yaliyopo kwenye msitu huo, ni kiburudisho kingine cha kukuongea ihai wa kuishi. Picha| K15 Photos.

Simu yako yenye uwezo kupiga picha nzuri basi itakupatia kumbukumbu nyingi za kufurahisha. Picha| K15 Photos.

Enable Notifications OK No thanks