Matokeo kidato cha nne mwaka 2020 haya hapa

Mwandishi Wetu 0135Hrs   Januari 15, 2021 Habari
  • Ufaulu waongezeka kwa asilimia 5.19.
  • Watahiniwa wa shule 373,958 wamefaulu mtihani kati ya wanafunzi 434,654 waliofanya mtihani huo.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2020 huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 5.19 kutoka ule wa mwaka 2019.

Necta imeeleza leo kuwa katika mtihani huo watahiniwa wa shule 373,958 wamefaulu mtihani kati ya wanafunzi 434,654 waliofanya mtihani huo Novemba mwaka jana ikiwa ni sawa na asilimia 85.84 ya watahiniwa wote. 

Hii ni sawa na kusema kuwa takriban wanafunzi 85 kati ya 100 waliofanya mtihani huo wamefaulu. 

Ufaulu huo, kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, ni sawa ongezeko la asilimia 5.19 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2019. Mwaka juzi asilimia 80.65 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo.


Soma zaidi:


Hata hivyo, ni wanafunzi 152,903 sawa na asilimia 35.1 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani huo wamefanikiwa kupata daraja la I hadi la III.

Kati ya wanafunzi hao waliopata ufaulu mzuri zaidi, wasichana ni 66,899.  


Kupata matokeo ingia hapa >>>>> https://bit.ly/2XIyOu0

Related Post