Maoni mchanganyiko matumizi ya sigara za kielektroniki Tanzania

Rodgers George 0611Hrs   Agosti 26, 2019 Maoni & Uchambuzi
  • Licha ya kutumika kama mbadala wa sigara za kawaida bado maswali yanabaki kwenye madhara. 
  • Baadhi ya watalaam wanasema zina madhara ya kiafya ambayo hayaonekani kirahisi.  
  • Watumiaji wa sigara hizo wanaohudhuria hospitali Marekani waongezeka.

Dar es Salaam. Kutokana na uwepo wa watumiaji wengi wa bidhaa za tumbaku, wanasayansi waliibuka na sigara ya kielektroniki “E-Cigarette” kama mbadala wa sigara za kawaida ili kuwapunguzia watumiaji madhara yanayoambatana na uvutaji wa sigara hizo.  

“E-Cigarette” Sigara hiyo ina fanyakazi kwa nguvu ya betri na kubadilisha nikotini iliyo kwenye mfumo wa kimiminika kuwa mvuke ambao mtumiaji huuvuta. 

Hakuna moto, hakuna majivu wala harufu ya moshi. Hapo awali iliaminika kuwa sigara hizo hazina kemikali zozote zinazohusiana na sigara za kawaida kama kemikali ya “tar” na “Carbon monoxide”.

Hata hivyo, baadhi ya wataalamu wameihusisha teknolojia hiyo kama njia ya kupunguza matumizi ya sigara huku wengine wakiona ni njia mojawapo ya kuchochea matumizi ya sigara kwani kampuni nyingi za sigara ndizo zinazohamasisha sigara hizo.

Katika siku za hivi karibuni, sigara hizo za kielektroniki zimekua gumzo hasa mtandaoni baada ya baadhi ya watumiaji wake kuhudhuria hospitali wakisumbuliwa na matatizo ya mapafu.

Kwa mujibu wa Idara ya Afya na Huduma za Binadamu ya Marekani kupitia Kituo cha Kudhibiti na kuzuia Magonjwa (CDC), hadi kufikia Agosti 21, 2019, watu 193 wameripotiwa kuwa na matatizo makubwa ya mapafu yakihusishwa na matumizi ya “E-cigarette” huko Marekani.

Tatizo hilo limeelezwa kuwasababishia wagonjwa hao ugumu kwenye kupumua na wengine kuwa na maumivu ya kifua.

Sigara hiyo ina fanyakazi kwa nguvu ya betri na kubadilisha nikotini iliyo kwenye mfumo wa kimiminika kuwa mvuke. Picha| Mtandao

Mwanafunzi katika Chuo cha Uuguzi na Udaktari KCMC, Mlemeta Chilala anasema kutumia sigara za kielektroniki kama mbadala wa sigara za kawaida bado siyo suluhisho kwani suluhisho ni kuacha kutumia sigara kabisa.

Chilala amesema uvutaji wa bidhaa za “Aerosal” zina madhara madogo na huchukua muda mrefu kuonekana ikilinganishwa na matumizi ya tumbaku ambayo ina kemikali kama “tar”, “carbonmonoxide” na “nicotine” ambazo zina viambata vya sumu.

“Uvutaji wake hauna data sana. Haieleweki madhara yake yapo kwa ukubwa gani. Wengine wanasema ina madhara, wengine wanasema madhara ni madogo ikilinganishwa na bidhaa za tumbaku,” amesema Chilala ambaye amewahi kumshuhudia mtu akitumia sigara hizo.


Zinazohusiana: 


Hata hivyo, wadau wa afya wamesema licha ya sigara za kielektroniki kutajwa kuwa na madhara madogo zikilinganishwa na sigara za kawaida, bado sigara hizo zina nikotini ambayo inaweza kumfanya mtu kuwa teja. 

Licha ya kuwa sigara hizo kuwa madhara kiafya, bado baadhi ya vijana hawazifahamu sigara hizo. 

Laurent Kaijage, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  (UDSM) ameiambia www.nukta,co,tz kuwa hafahamu madhara zaidi ya sigara hizo tofauti na anayoyaona mtandaoni.

“Niliwahi ona mtandaoni sigara hiyo ikimlipukia mtu. Sifahamu zaidi wala sijawahi ona mtu akitumia,” amesema Kaijage.

Related Post