Mambo ya kufanya kulinda afya ya macho yako
April 19, 2021 9:19 am ·
Rodgers Raphael
- Ni pamoja na kuepuka kutumia dawa bila maelekezo ya daktari.
- Unashauriwa kupima macho mara kwa mara.
Dar es Salaam. Kadiri umri unavyozidi kusogea uzeeni, viungo vya mwili taratibu huanza kupungukiwa uwezo wake wa kufanya kazi. Kuanzia miguu, mgongo na vivyo hivyo kwa macho.
Hata hivyo, kwa namna moja ama nyingine, tabia zetu za kila siku zinaweza kuharakisha au kupunguza kasi ya kupungua kwa uwezo wa kuona.
Kwa mujibu wa Daktari na Mtafiti kutoka Taasisi ya Afya ya Jamii (KCMUco), Dk Julieth Sebba, yapo mazoezi au tabia nzuri zinazoweza kuifanya afya ya macho yako kuwa nzuri kadri umri wako unavyozidi kusogea.
Epuka matumizi ya sigara, dhibiti magonjwa kama kisukari na presha ya damu na epuka matumizi ya dawa za macho bila ushauri wa mtaalamu wa afya.
Kufahamu zaidi, tazama video hii:
Latest

11 hours ago
·
Fatuma Hussein
Rais Samia amtwisha zigo bosi mpya Tanesco
1 day ago
·
Fatuma Hussein
Wizara ya Mifugo na Uvuvi yaomba bajeti ya Sh476.65 2025/26

2 days ago
·
Fatuma Hussein
Tumia viwango hivi kubadili fedha za kigeni Mei 23, 2025

4 days ago
·
Kelvin Makwinya
Polisi yawasaka wadukuzi baada ya kuzua taharuki mtandaoni