Karatasi zisizotumika ofisini ni ‘dili’ kwa vijana

February 11, 2019 9:31 pm · Zahara
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanazikusanya na kuzipanga kwa mafungu ili kuzirejeza na kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo karatasi laini na mapamba ya nyumbani.
  • Ni ajira kwa vijana wanaopenda uhifadhi wa mazingira.  

Dar es Salaam. Wakati unawaza kutupa taka za karatasi au kuzichoma moto zinapokuwa nyingi ofisini, wenzako wanaziona kama fursa ya kuzirejeza au kuzibadilisha ili ziweze kutumika katika maeneo mengine na kusaidia katika uhifadhi wa mazingira.

Kampuni unayochipukia ya Zaidi ya jijini Dar es Salaam ambayo inafanya kazi ya urejelezaji taka wamekuja na kampeni ya ‘TakaNiAjira’ ambayo wanakusanya mabaki ya karatasi kutoka taasisi na mashirika mbalimbali ili kutengeneza karatasi laini (Tissue na Toilet Papers).

‘TakaNiAjira’ inaweza pia kuwa suluhisho kwa ofisi zilizohifadhi nyaraka zisizotumika lakini hawajui kwa kuzipeleka. Wao wanafika mpaka katika mlango wa ofisi yako na kuzichukua kwa ajili ya matumizi mengine yenye faida.

Kampeni hiyo inalenga kuondoa changamoto ya uchafuzi wa mazingira hasa kuzagaa kwa taka au hewa chafu inayotokana na uchomaji wa karatasi.

Ofisi zinaweza kuepuka uchafu kwa kuwapa vijana wanaoweza kuzitumia kwa shughuli nyingine ya kuzalisha bidhaa ili kulinda mazingira. Picha|Zahara Tunda.

Afisa Masoko wa kampuni hiyo, Emanuel Mgelwa amesema jukumu walilonalo sasa ni kutoa elimu katika ofisi mbalimbali juu ya utunzaji wa mazingira katika maeneo yao na kukusanya karatasi ambazo hazina matumizi endelevu. 

“Huwa tunatoa elimu kuhusu uhifadhi wa karatasi hizo, na baada ya hapo tunasambaza dustbin (mapipa ya taka) za kuwekea uchafu katika taasisi mbalimbali ambazo zina watu wengi,” amesema Mgelwa.


Zinazohusiana: 


Mpaka sasa kampeni hiyo inayoendeshwa na vijana zaidi ya 30 imefanikiwa kuyafikia mashirika mbalimbali ikiwemo Shirika la Misaada ka Marekani (USAID), COWI, StarTimes, shule ya sekondari ya Jangwani na Azania za jijini za Dar es Salaam.

Licha ya kampeni kuwa na matokeo chanya,bado wanapata changamoto ya sera za baadhi ya mashirika kutokuruhusu nyaraka zao kutumika kwa matumizi mengine nje ya ofisi. 

                       

Kuhusu soko la taka wanazozikusanya kuzipanga katika mfumo wa madaraja na kuziuza katika Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi Paper Mills na Tanpack Tissues Limited cha jijini Dar es Salaam ili kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo karatasi laini.

Hata hivyo, Zaidi sio kampuni pekee iliyo mstari wa mbaele kutunza mazingira jijini hapa, wapo vijana ambao wameamua kujiajiri kukusanya matairi ya magari, chupa za pombe kali na mvinyo, chupa na mifuko ya plastiki na kutengeneza bidhaa mbalimbali yakiwemo mapambo na urembo wa nyumbani. 

Enable Notifications OK No thanks