Haya ndiyo maeneo yanayotembelewa zaidi na watalii duniani

May 2, 2019 9:00 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Maeneo hayo yamebeba historia na ni alama muhimu ya mataifa makubwa duniani ya Marekani, Italia, Ufaransa, Uingereza na Hispania.
  • Mnara wa Effeil uliopo katika jiji la Paris, Ufaransa na sanamu ya Uhuru iliyopo Marekani ni miongoni mwa maeneo yanayotembelewa zaidi na watalii duniani.

Dar es Salaam. Kila nchi duniani ina upekee wake. Upekee huo unaweza kuwa ni vivutio vya utalii ambavyo hulifanya eneo kuwa maarufu. 

Vivutio hujumuisha fukwe, hoteli za kifahari, milima, wanyama wa porini na kufugwa, majengo ya kihistoria na hata uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia ya kisasa katika shughuli za uzalishaji. 

Vivutio vya utalii hutumika kama alama za utambulisho kimataifa ambazo huvuta watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani. Mfano mlima Kilimanjaro ni alama muhimu inayoitambulisha Tanzania kimataifa kwa sababu ni mlima mrefu kuliko yote Afrika. 

Lakini yapo maeneo duniani ambayo yamebeba maajabu ambayo huvuta hisia za watu wengi, kiasi kwamba shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO) huyatambua na kuyatenga maeneo hayo kama sehemu muhimu ya urithi wa duniani. 

Kwa mujibu wa tovuti ya TripAdvisor inayowaunganisha watalii na vivutio duniani inaeleza kuwa miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa zaidi na watalii mwaka 2018 ni pamoja na Sanamu ya Uhuru (Statue of Liberty) iliyopo New York, Marekani; Makumbusho ya Vatican (Italia); Mnara wa Effeil (Paris, Ufaransa); Mawe yaliyosimama ya Stonehenge (Wiltshire, Uingereza); na kanisa la Lagrada Familia (Barcelona, Hispania).

Enable Notifications OK No thanks