Google Fusion Tables kuzikwa rasmi Desemba 3
- Kampuni ya teknolojia ya Google imesema ifikapo Desemba 3, 2019 itaifunga rasmi programu tumishi ya Google Fusion Tables iliyokuwa inatumiwa kuchambua data na kusanifu michoro mbalimbali.
- Katika kipindi cha miezi mitatu iliyobaki, Google imewashauri watumiaji wa programu hiyo, kuamisha nyaraka na kazi zao ili kuepuka usumbufu wakati itakapoondolewa sokoni rasmi.
Kampuni ya teknolojia ya Google imesema ifikapo Desemba 3, 2019 itaifunga rasmi programu tumishi ya Google Fusion Tables iliyokuwa inatumiwa kuchambua data na kusanifu michoro mbalimbali.
Katika kipindi cha miezi mitatu iliyobaki, Google imewashauri watumiaji wa programu hiyo, kuamisha nyaraka na kazi zao ili kuepuka usumbufu wakati itakapoondolewa sokoni rasmi.
Hata hivyo, Google imetoa njia ya kuwasaidia wateja wake kwa kuwapatia zana (tool) ijulikanayo kama “Google Takeout” kwa ajili ya kuhamisha nyaraka zao ili zisipotee bila kujali wingi wake kwani imewekwa kirahisi kuzihamisha kupitia programu hiyo.
Unaweza kuzirekodi hizo data kwa mifumo tofauti kati ikiwemo “JavaScript Object Notation” (JSON), “Comma-separated values” (CSV) na “Keyhole Markup Language” (KML).
Soma zaidi:
Programu hii ilianzishwa Juni 9, 2009 na imekuwa ikitumika zaidi na Waandishi wa habari za takwimu kwa ajili ya kukusanya, kutengeneza na kutuma takwimu kwa njia ya mbalimbali ikiwemo majedwali.
Wakati wanafunga mifumo yote inayoingiliana na programu hiyo ifikapo tarehe husika ambapo watumiaji wote wataanza kuona jumbe (error message) katika data zote zitakazokuepo kwenye programu hiyo.
Kama Google itafanikiwa kuizika rasmi Google Fusion Tables basi ni itakuwa imeziondoa rasmi sokoni programu zake mbili katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kuifuta Google Plus Februari 4, 2019.