Google yaingiza sokoni mtandao mpya wa kijamii
- Unajulikana kama Shoelace na umeanza kwa majaribio katika mji wa New York, Marekani.
- Umebuniwa takriban miezi mitatu tangu mtandao wa Google+ ifungwe.
- Unafanya kazi kwa watumiaji wa simu za Android and Apple wenye akaunti ya Google.
Kampuni ya teknolojia ya Google imeanzisha jukwaa jipya la mtandaoni lenye lengo la kuwaleta pamoja watu wenye mtazamo sawa kupitia matukio mbalimbali au vitu wanavyovipenda.
Hatua hiyo imekuja Ikiwa ni miezi mitatu tangu kampuni hiyo ya Marekani ilipotangaza kuufunga mtandao wake wa Google + Aprili mwaka huu.
Jukwaa hilo litakuwa linaendeshwa na rrogramu tumishi ya simu iliyopewa jina la Shoelace ambapo itakuwa inafanya kazi ya kumshauri mtu kila siku kuhusu tukio linalotokea karibu yake ikiwemo maonyesho ya bure au michezo mbalimbali inayofanyika karibu na eneo analoishi.
Kwa sasa Shoelace inafanyiwa majaribio katika Jiji la New York na unapatikana kwa watu wachache kupitia kitengo cha Google kinachohusika na majaribio cha Google Area 120.
Zinazohusiana:
“Lengo kubwa la kuanzishwa kwa Shoelace ni kuwakutanisha watu pamoja hasa wale wenye malengo au vitu vinavyofanana,‘’ imesema sehemu ya taarifa ya Google kwenye tovuti ya shoelace.
Lakini watakaohitaji mtandao huo kuwafikia katika maeneo yao wanatakiwa kuomba ‘code’ maalum ili kupata huduma hiyo.
Programu tumishi hiyo inafanya kazi katika simu za Android kuanzaa kuanzia toleo la v.8.0 na simu mpya ambapo watumiaji wa simu za Apple kuanzia toleo la v.11.0 na mpya zaidi ya hapo. Kigezo kingine cha kutumia mtandao huo ni lazima uwe na akaunti ya Google.
Hata hivyo, mtandao huo utaweza kushindana na kujipatia wafuasi wengi kama ilivyo kwa Facebook, Instagram na WhatsApp ambayo imetawala soko la mitandao ya kijamii duniani.