Fanya haya kurahisisha safari yako

January 29, 2020 1:29 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Kama una safari hivi karibuni na begi lako halitoshi, viringisha nguo zako ili kupata nafasi ya ziada.
  • Fanya utafiti kufahamu sehemu unayoenda.
  • Ni busara kuyafahamu mahitaji ambayo ni ya lazima pekee na siyo kubeba vitu ambavyo huenda usivitumie.

Dar es Salaam. Kama una mpango wa kusafiri kwa ajili ya shughuli za kikazi, biashara au mapumziko na bado hujui hujaweka vitu vyako vizuri kwenye begi, usihofu

Dondoo hizi zitakusaidia kupanga vitu vyako vyote vya safari zikiwemo nguo kwenye begi na kukuhakikishia safari yako inakuwa yenye furaha na mafanikio makubwa. 

Viringisha nguo zako badala ya kuzikunja

Kama umewahi kupata safari ambayo inakutaka ubebe nguo nyingi lakini ukiangalia kwenye hifadhi ya mabegi yako hakuna linalotosha nguo hizo, ni dhahiri utakua unaelewa ninachoongelea.

Ni vema ukafahamu kuwa, unapokunja nguo, inachukua nafasi kubwa zaidi na hivyo kukupa uwanda mdogo wa kupaki nguo zako.

Kama una nguo nyingi na begi lako halitoshi, unaweza anza kuviringisha nguo zako pale unapokuwa umezikunja na kisha utaona jinsi gani nafasi inabaki kwenye begi lako.

Beba nguo zinazohitajika tu katika safari yako. Picha|Mtandao.

Funga mafuta na vimiminika kwenye kifungashio cha nailoni

Ni mara ngapi umefika safarini na kukuta nguo zako zimeloa mafuta ambayo huenda yalifunguka kutokana na mgandamizo?

Anza kutatua changamoto hiyo kwa kuvifungasha vitu hivyo kwenye mfuko wa nailoni ili kuepuka changamoto hiyo. Itakusaidia kukuepusha na gharama za kufua ufikapo safarini hasa hotelini.

Ukifika unakokwenda, toa kitu unachotumia tu

Ni kweli hoteli zina makabati na sehemu za kuwekea nguo lakini pale siyo nyumbani kwako.

Ili kuepuka kusahau baadhi ya vitu vyako ambavyo ni muhimu kutokana na haraka au dharula, ni vema ukatoa kitu kwenye sanduku lako au begi endapo unahitaji kukitumia tu.

Zaidi, itakusaidia katika ulazima wa wewe kutumia muda mwingi kwenye kufungasha tena kwa ajili ya safari yako ya kurudi nyumbani.


Soma zaidi:


Paki kwa malengo

Unasafiri tu, hauhamii huko uendako hivyo ni vizuri kuchukua vitu vya muhimu pekee mfano kwa manaume, sio lazima kubeba nguo nyingi kwa safari ambayo ni ya wiki moja. 

Andaa orodha ya mahitaji yako unayohitaji kusafiri nayo na kisha anza kuweka alama kimoja baada ya kingine hadi umalizapo.

Furahia safari yako kwa kubeba vitu vichache vitakavyofanikisha safari yako. Picha|Mtandao.

Hakikisha unafahamu walau kwa kiasi sehemu unayoenda

Kama haufahamu mahali unapokwenda, ni busara kufanya utafiti kuhusu sehemu hiyo kwani itakupatia uwanda wa mahitaji ambayo unahitaji ukiwa huko. Kuna sehemu ambazo zipo mbali na maduka pamoja na huduma zingine za muhimu ambazo kwa hakika unahitaji kuwa nazo.

Ni vyema ukafanya utafiti huo ili kuepukana na kushindwa kupata huduma ambazo za muhimu zikiwemo dawa mbalimbali.

Tunaendelea kukuletea madini ambayo ni muhimu zaidi katika maisha yako ya kila siku. Usiakae mbali na ukurasa huu.

Enable Notifications OK No thanks