Epuka kupigwa: Vodacom haigawi hela za Corona

June 1, 2020 10:43 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Puuza ujumbe unaozagaa kwenye mitandao ya kijamii ikidai Vodacom M-pesa inatoa Sh80,000 kwa wateja wake kwa ajili ya COVID-19.

Dar es Salaam. Baadhi ya watumiaji wa mtandao  wamejikuta wakipokea ujumbe wa uzushi uliokuwa ukitangaza neema bandia ya kupatiwa Sh80,000 kutoka Vodacom Tanzania ikidaiwa kuwa ni ahueni ya kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19).

Tangu mapema Mei 31 kumekuwa na ujumbe ukisambaa kwenye mitandao ya kijamii ukidai kwamba kampuni ya simu ya Vodacom inagawa pesa kupitia M-pesa ikiwa ni  “ni sehemu ya ukarimu wao kwa kusaidia raia wakati wa janga hili.”

Ukweli ukoje

Taarifa hizo ni uzushi na kama kujipanga kupunguza uchungu wa maisha na pesa hizo fikiria.

Kutokana na kusambaa kwa habari hizo, Vodocam leo Mei 31 ,2020 imekanusha taarifa hiyo inayosambaa kwenye mtandao ya kijamii yenye kichwa cha habari “Hela za Covid kutoka Vodacom”.

“Taarifa hii siyo ya kweli na yenye nia ya utapeli.Tunakuhimiza yeyote utakayepata taarifa hiyo uipuuze na tafadhali usiisambaze kwa watu wengine,” imesema sehemu hiyo ya taarifa ya Vodacom.

Taarifa hiyo ni miongoni mwa maelfu ya taarifa za uzushi ambazo zimekuwa zikisambaa wakati huu ambao Taifa linakabiliana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19).

Enable Notifications OK No thanks