Bidhaa za bia, juisi za unga kutozwa ushuru 2020-21
June 11, 2020 2:13 pm ·
Rodgers Raphael
- Bidhaa hizo ni juisi na bia za unga zinazoingizwa kutoka nje ya nchi
- Bidhaa ya juisi zinapendekezwa kutozwa zaidi ya Sh 232 huku bia za unga zikipendekezwa kutozwa zaidi ya Sh800.
Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amependekeza kufanya marekebisho ya kutoza ushuru wa bidhaa za bia na juisi za unga ambazo zinaingizwa kutoka nchi za nje.
Amesema lengo la mabadiliko hayo ni kupanua wigo wa kodi kwa kuwa bidhaa hizo zinaagizwa kwa wingi kutoka nje ya nchi.
Zinazohusiana
- Uchumi wa Tanzania kukua kwa asilimia 5.5 mwaka 2020
- Yaliyochangia uchumi wa Tanzania kukua kwa asilimia 7.2 robo ya pili 2019
- Wizara sita zitakazotumia fedha nyingi bajeti 2020-21
Kwa upande wa bia za unga, waziri huyo amependekeza bidhaa hiyo itozwe ushuru kwa kiwango cha Sh844 kwa kilo na juisi ya unga (Sh232)
“Hatua za kutoza ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa zisizo za petroli kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 45.8,” amesema Dk Mpango leo wakati akiwasilisha bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2020/21.
Latest

2 hours ago
·
Esau Ng'umbi
Riba ya benki kuu Tanzania yabakia 6% kwa mara ya nne mfululizo

8 hours ago
·
Fatuma Hussein
Tumia viwango hivi kubadili fedha za kigeni Aprili 4,2025

24 hours ago
·
Kelvin Makwinya
Waliofanya usaili wa maandishi TRA kujua mbivu na mbichi Aprili 25

2 days ago
·
Lucy Samson
Serikali yawaita wahitimu wa kidato cha nne kubadili tahasusi, chuo