Rais Samia ahimiza umuhimu wa michezo kukabiliana na magonjwa

August 14, 2025 7:31 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema michezo itasaidia kukabiliana na magonjwa hayo yanayosababishwa na mtindo mbaya wa maisha.

Arusha. Rais Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Nishani ya Heshima ya Juu ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (The Grand Cordon) huku akiwataka Waafrika kushiriki katika michezo mbalimbali ili kukabiliana na magonjwa ikiwemo yasiyoambukiza

Rais Samia aliyekuwa akizungumza baada ya kutunukiwa nishani na Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) Ikulu Dar es Salaam leo Agosti 14,2025 amesema kuwa michezo itasaidia kukabiliana na magonjwa hayo yanayosababishwa na mtindo mbaya wa maisha ikiwemo kutokufanya mazoezi.

“kwa kutambua kuwa kushiriki katika michezo hujenga afya bora ni muhimu kuendelea kuongeza uwekezaji kwa wote ili tuwe na wananchi wenye afya bora lakini kwa mnasaba wa shughuli ya leo ili tuwe na Afrika yenye wananchi wenye afya njema.

Kwa sababu Afrika sasa hivi ni bara linalotambulika na kupanda kwa nguvu duniani kiuchumi, utulivu wa kisasa na kwamba Afrika ndiyo inayotegemewa na dunia kwenye ‘food security’ na mambo mengine hivyo ni vyema kuwa na Waafrika wenye nguvu na wenye afya ili tuweze kutoa huduma ndani ya dunia yetu,”amesema Rais Samia.

.Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa CISM Kanda ya Afrika Meja Jenerali Maikano Abdullahi kutoka Nigeria mara baada ya kutunukiwa Nishani ya Heshima ya Juu ya Baraza la Michezo.Picha/Ikulu

Shirika la Afya Duniani (WHO) linayataja magonjwa yasiyoambukiza kuwa ni saratani, magonjwa ya moyo,kisukari, pamoja na magonjwa ya mfumo wa upumuaji ambayo huwaathiri sana watu wenye vipato vya chini na vya kati.

Kwa mujibu wa shirika hilo Magonjwa hayo yalisababisha vifo ya watu milioni 43 mwaka 2021 sawa na asilimia 75 ya vifo vyote vinavyotokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza vilivyotokea duniani.

Ili kupambana na magonjwa hayo Rais Samia amemuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Palamagamba Kabudi mubuni mbinu zinatazoongeza ushiriki thabiti na uwekekzaji katika miundombinu ya michezo.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kutunukiwa nishani hiyo akimtaja kama kiongozi wa kipekee na wa kuigwa barani Afrika.

Kwa mujibu wa Dk Stergomena, heshima hiyo si tu inatambua mchango wa Rais Samia katika kuendeleza michezo ya majeshi, pia inaweka alama ya kihistoria. Tangu kuanzishwa kwa nishani hiyo mwaka 1952, Rais Samia amekuwa kiongozi wa saba duniani na wa kwanza mwanamke barani Afrika kuipokea.

“Tuna kila sababu ya kujivunia. Hii ni heshima kubwa kwa Taifa letu na inathibitisha namna Rais wetu anavyotambuliwa kimataifa kwa mchango wake katika kuimarisha ushirikiano wa michezo ya majeshi,” amesema Dk Stergomena

.Nishani hiyo hutolewa na CISM kwa viongozi wa nchi wanaoonyesha mchango wa kipekee katika kuendeleza michezo ya kijeshi na kuimarisha mshikamano wa kimataifa kupitia michezo

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV