Rais Magufuli awajia juu TRA, awataka wabuni vyanzo vipya vya kodi

April 2, 2019 4:33 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Rais John Magufuli akimuapisha Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha|Michuzi blog.


  • Amesema haridhishwi na utendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika ukusanyaji wa kodi na kuitaka mamlaka hiyo kutanua wigo wa walipa kodi kwa kubuni vyanzo vipya vya kodi na kujenga mazingira rafiki ya watu wengi kulipa kodi. 
  • Ameeleza kutofurahishwa na mrundikano  wa kesi za kodi mahakamani na ametaka tatizo hilo lifanyiwe kazi na mamlaka husika.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema haridhishwi na utendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika ukusanyaji wa kodi na kuitaka mamlaka hiyo kutanua wigo wa walipa kodi kwa kubuni vyanzo vipya vya kodi na kujenga mazingira rafiki ya watu wengi kulipa kodi. 

Rais Magufuli aliyekuwa akizungumza leo (Aprili 1, 2019) Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumuapisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Fedha na Mipango atakayeshughulikia sera, Adolf Ndunguru na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Mapato Tanzania (TRA) Msafiri  Mbibo amesema mpaka sasa walipa kodi wanaotambulika rasmi na TRA ni 2.7 milioni tu kati ya watanzania zaidi ya 55 milioni ambapo inawaumiza walipa kodi wachache kwa kuwapangia viwango vikubwa vya kodi. 

Amesema TRA ina uwezo wa kupanua wigo wa ulipaji kodi kwa kuweka viwango vya kodi vitakavyowavutia walipa kodi wengi lakini imeshindwa badala yake inawakamua walipa kodi wachache. 

“Ukienda mipakani wafanyabiashara wanafungua maduka upande nchi za wenzetu na siyo upande wa Tanzania, na sababu kubwa ni kwamba wakifungua upande wa Tanzania wanasumbuliwa na TRA, wekeni viwango vya kodi vinavyolipika ili watu wengi waweze kulipa kodi badala ya kukwepa” amesisitiza Rais.

Amesema TRA wanapaswa kubuni vyanzo vipya vya kodi na kuhakikisha wanatengeneza mazingira mazuri yatakayovutia watu wengi kulipa kodi. 


Soma zaidi:


Hata hivyo, ameeleza kutofurahishwa na mrundikano  wa kesi za kodi mahakamani na ametaka tatizo hilo lifanyiwe kazi kwa kuwa linasababisha kodi nyingi kutolipwa kwa kusubiri mivutano ya kesi na kuwataka Mbibo na Ndunguru kurekebisha dosari zilizopo katika ofisi zao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa watumishi wanaoonekana ni kikwazo cha kutekeleza mipango yao.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais Sarnia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk  Ashatu Kijaji, Makatibu Wakuu, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Mama Samia amesema viongozi hao wanatarajiwa kufanya vizuri zaidi katika nafasi walizopewa hivi sasa hasa ikizingatiwa kuwa wanakwenda kufanya kazi katika ofisi zenye mchango mkubwa katika uchumi wa nchi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV