Rais Magufuli atangaza siku nne za maombelezo ya waliofariki katika ajali ya Mv Nyerere

September 21, 2018 10:01 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Rais amesema  katika kipindi hicho cha maombolezo, anaamini kila mtu kwa imani yake atawaombea marehemu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametangaza siku nne za maombolezo kuanzia leo (Septemba 21) hadi 24, 2018 kuwakumbuka waliopoteza maisha katika ajali mbaya ya kivuko cha Mv Nyerere kulichozama katika Ziwa Victoria jana mchana na kuua watu zaidi ya 131 hadi sasa.

Dk Magufuli, aliyekuwa akilihutubia taifa kupitia TBC1 na TBC Taifa, amesema  katika kipindi hicho cha maombolezo, anaamini kila mtu kwa imani yake atawaombea marehemu waliopoteza maisha katika ajali hiyo mbaya kutokea katika siku za hivi karibuni.

                     

Rais John Magufuli akihutbia Taifa baada ya kutokea ajali ya Mv Nyerere katika Ziwa Victoria. Video| Ikulu.

Mapema leo Saa 10 jioni, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Kanali Lucas Magembe aliiambia Nukta kuwa hadi wakati huo watu 126 walikuwa wameopolewa wakiwa wamafariki huku idadi ya waliohai ikiwa ni 37. Hata hivyo, Kijazi anasema watu 40 wameokolewa wakiwa hai.

Kanali Magembe amesema kuwa uokoaji unaendelea na kwamba baadhi ya majeruhi waliokuwa wamelazwa katika Kituo cha Afya ya Bwisya wameanza kuruhusiwa baada ya kupata nafuu.

Kutokana na ajali hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshawasili kisiwani Ukara kuungana na viongozi wengine wanaosimamia jitihada za uokoaji katika eneo hilo la tukio.

Kituo cha televisheni cha Taifa, TBC1 kimemuonyesha Majaliwa akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

Majaliwa amelazimika kusitisha ziara yake ya siku saba iliyokuwa ikiendelea katika mkoa wa Dodoma, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu iliyotolewa leo mchana.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV