Rais Magufuli amkaribisha Putin Tanzania

March 14, 2019 8:27 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na ujunbe wa Urusi ulioongozwa na mjumbe maalum wa Rais wa Urusi Vladimir Putin katika masuala Afrika ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo Nje, Mikhail Bogdanov leo (Machi 13, 2019) Picha| lkulu Jijini Dar es Salaam.


  • Amemkaribisha na wawekezaji wa nchi hiyo kutembelea nchiini ili kuwekeza katika fursa mbalimbali zilizopo.
  • Dk Magufuli amesema Tanzania inatambua umuhimu wa ushirikiano na Urusi itakuza na kuendeleza uhusiano katika masuala ya biashara, uwekezaji, utalii na utoaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya, elimu na miundombinu. 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemkaribisha Rais wa Urusi Vladimir Putin na wawekezaji wa nchi hiyo kutembelea Tanzania ili kuwekeza katika fursa mbalimbali zilizopo nchini. 

Amesema Tanzania inatambua umuhimu wa ushirikiano uliopo kati yake na Urusi ina itaendeleza na kuimarisha katika masuala ya biashara, uwekezaji, utalii na utoaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya, elimu na miundombinu. 

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Urusi ulioongozwa na mjumbe maalum wa Rais Putin katika masuala Afrika ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo Nje, Mikhail Bogdanov leo (Machi 13, 2019) lkulu Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema Watanzania wanaipenda Urusi na anamkaribisha rais huyo atembelee Tanzania.

“Naomba ufikishe ujumbe wangu kwa Rais Putin kuwa Watanzania wanaipenda Urusi na tunamkaribisha kuja kutembelea nchi yetu pamoja na wananchi wengine wa Urusi, tunawakaribisha pia wawekezaji waje wawekeza katika fursa mbalimbali zilizopo hapa Tanzania kwa manufaa yetu sote,” amesema Rais Magufuli katika taarifa iliyosainiwa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu. 

Naye Bogdanov, ambaye amewahi kutembelea Tanzania miaka nane iliyopita, ameipongeza Serikali kwa kasi nzuri ya maendeleo iliyopata katika kipindi kifupi na amebainisha kuwa Urusi imedhamiria kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania.


Soma zaidi: Magufuli aangazi rada kuongeza mapato Tanzania


Amesema Urusi ina mpango mahususi wa kushirikiana na nchi za Afrika ikiwemo Tanzania katika kuongeza kasi ya maendeleo na kuwa hivi karibu Tanzania na Urusi zitatiliana saini makubaliano ya kuanzisha tume ya pamoja ya ushirikiano (WM Permanent Commission-JPC) katika biashara, uwekezaji na uchumi ili rasilimali na fursa zilizopo katika pande zote zitumike kwa manufaa wananchi wa nchi hizo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema tume hiyo itakayoanzishwa itasaidia  kukuza uchumi kupitia madini, gesi na utalii hasa wakati huu ambapo Urusi imeitazama Tanzania kuwa nchi yenye vivutio bora vya utalii duniani.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.