Precision Air yasitisha safari za ndege Nairobi

February 17, 2026 4:11 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kutokana na mgomo unaoendelea jijini Nairobi Kenya.
  • KCAA yaagiza kurejeshwa kwa usafiri wa anga.

Arusha.Shirika la Ndege la Precision Air limetangaza kusitisha safari zake zote za kuingia na kutoka jiji la Nairobi kufuatia mgomo wa Chama cha Wafanyakazi wa Usafiri wa Anga nchini Kenya (KAWU).

Mgomo huo unaoshuhudiwa kwa siku ya pili katika uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) ambao ni miongoni wa mwa viwanja vyenye shughuli nyingi zaidi barani Afrika umesababisha mamia ya abiria kukosa usafiri huo muhimu.

Taarifa ya Precision Air iliyotolewa leo Februari 17, 2026 imetangaza kusitishwa kwa shughuli zote za usafiri kwa siku ya leo ikiwaomba radhi abiria wanaotumia shirika hilo.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote unaoweza kujitokeza. Kwa abiria walioathirika, timu yetu inafanya kazi kwa haraka kupanga chaguo mbadala la safari.

…Tunaendelea kufuatilia hali hii kwa karibu na tutatoa taarifa zaidi kadiri itakavyopatikana,” imesema taarifa ya Precision Air iliyochapishwa katika ukurasa wa Instagram.

Baadhi ya abiria waliokwama katika Uwanja wa Ndehe wa Kimataifa Jomo Kenyatta baada ya usafiri wa ndege kusitishwa.Picha /Reuters.

Aidha, Shirika  hilo limewashauri abiria kuangalia barua pepe na ujumbe mfupi (SMS) mara kwa mara kwa taarifa mpya, kuepuka kwenda uwanja wa ndege kabla ya kuthibitisha hali ya ndege anayotarajia kupanda pamoja na kuhakikisha mawasiliano yao yamesasishwa (updated).

Pamoja na hayo abiria wametakiwa kuwasiliana na shirika hilo kwa namba za simu +255 746 984 100 / +255 784 108 800 au barua pepe kwa anwani ya contactcentre@precisionairtz.com.

KCAA yaagiza kurejeshwa kwa usafiri wa anga

Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Kenya (KCAA) imetangaza kufanya mkutano na umoja wa wafanyakazi hao na kuagiza shughuli za usafiri wa anga zirejeshwe mara moja.

Taarifa  ya KCAA iliyotolea mchana wa leo inabainisha kuwa tayari viongozi wa Serikali pamoja na viongozi wa chama hicho wamefanya mazungumzo na kukubaliana kurejesha shughuli  hizo mara moja.

“Pande zote zilikubali rasmi kurejea kazini mara moja. “Usafiri wa anga unachangia pakubwa katika uchumi wa nchi na tumejitolea kuhakikisha kuwa sekta hii inabakia kuwa tulivu,”  imesema taarifa hiyo ikimnukuu Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Kenya Davies Chirchir.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.