Polisi yamkamata aliyetishia, kujeruhi kwa bastola Dar es Salaam

October 28, 2024 1:02 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema taratibu za kumfikisha mtuhumiwa katika hatua nyingine za kisheria zinaendelea.

Arusha. Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linamshikilia Derick Junior (36) Mkazi wa Salasala, Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujeruhi na kutishia kwa silaha.

Taarifa ya Jeshi la Polisi inakuja wakati ambao video inayomuonesha mtuhumiwa aliyetambulika kuwa Derick akimshambulia na kumjeruhi mtu mwingine na silaha aina ya bunduki kusambaa katika mitandao ya kijamii jambo lililoibua mijadala na hisia mseto.

Kwa mujibu wa polisi baada ya uchunguzi jeshi hilo lilibaini tukio hilo lilifanyika Oktoba 27, 2024 saa 12.30 asubuhi maeneo ya Masaki ‘1245 night club’ Kinondoni ambapo mtuhumiwa alimjeruhi Julian Bujuru kwa kumpiga na kitako cha bastola pia kumjeruhi sehemu ya jicho na pua.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam Jumanne Murilo leo Oktoba 28, 2024 inaeleza kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa na taratibu za kumfikisha katika hatua nyingine za kisheria zinaendelea

“Aidha Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka linakamilisha utaratibu wa kisheria ili mtuhumiwa aweze kufikishwa katika Vyombo vingine vya Sheria haraka iwezekanavyo,” imesema taarifa ya Murilo.

Katika hatua nyingine jeshi hilo limesema halitasita kumchukulia hatua mtu yoyote anayemiliki silaha atakayebainika kufanya matendo ambayo ni kinyume na sheria kanuni na taratibu zilizoainishwa katika kibali chake cha kumiliki silaha.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV