Petroli, mahindi vyachangia kushusha mfumuko wa bei Tanzania

October 8, 2020 12:16 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Umeshuka baada ya kung’ang’ania katika kiwango cha asilimia 3.3 kwa miezi miwili mfululizo. 
  • Umeshuka hadi asilimia 3.1 kwa mwaka ulioishia Septemba 2020 kutoka asilimia 3.3 iliyorekodiwa mwaka ulioishi Agosti mwaka huu.
  • Umechagizwa na kupungua kwa gharama za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

Dar es Salaam. Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini Tanzania imeshuka hadi kufikia asilimia 3.1 kwa mwaka ulioishia Septemba 2020 kutoka asilimia 3.3 iliyorekodiwa mwaka ulioshia Agosti 2020, ikichagizwa na kupungua kwa gharama za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

Kushuka kwa mfumuko wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Septemba 2020 kumekuja baada ya kasi yake kung’ang’ania katika kiwango kimoja kwa miezi miwili mfululizo. 

Mwezi uliopita NBS ilieleza kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Agosti 2020 ulikuwa asilimia 3.3 ikiwa ni sawa kabisa na kiwango kilichorekodiwa katika mwaka ulioishia Julai 2020.

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Ripoti ya mfumuko wa bei ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) iliyotolewa leo Oktoba 8, 2020, imeeleza kuwa kushuka kwa mfumuko wa bei katika mwezi Septemba 2020 kumechangiwa na kupungua kwa baadhi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula ikilinganishwa na mwezi Septemba 2019.


Soma zaidi: 


Mfumko wa bei  wa bidhaa zisizo za chakula ambazo umeshuka ni pamoja na mafuta ya taa ambayo yameshuka kwa asilimia 15.6, dizeli (asilimia 14.2) na petroli kwa asilimia 10.2.

“Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizopungua bei kwa mwezi Septemba 2020 zikilinganishwa na mwezi Septemba 2019 ni pamoja na mchele kwa asilimia 2, mahindi kwa asilimia 10.2, unga wa ngano kwa asilimia 1.3, mihogo kwa asilimia 18.4 na viazi vitamu kwa wasilimia 10.7,” inaeleza sehemu ya taarifa ya NBS.

NBS imeeleza kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Septemba 2020 umepungua hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2020.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.