Orodha ya matukio, watu maarufu waliotikisa mtandao wa Twitter 2019
- Orodha hiyo ya 10 bora ya mijadala ilitawala zaidi katika mtandao huo mwaka 2019.
- Orodha hiyo ni ya matukio, mada, watu maarufu, #hashtag na emoji.
Mtandao wa Twitter umetoa orodha yake ya matukio, mada, watu maarufu, #hashtag na emoji ambazo zilijadiliwa na kuteka zaidi mazungumza ya mtandao huo kwa mwaka 2019 na kuleta matokeo tofauti kwenye jamii ikiwemo kuongeza uhuru wa kutoa maoni.
Orodha hiyo inajumuisha 10 bora ya watu au matukio yaliyoshikilia nafasi za juu katika kujadiliwa na kupata umaarufu katika mtandao huo.
Kwa upande wa wanasiasa ambao walijadiliwa zaidi mwaka huu katika mtandao huo ni Rais Donald Trump wa Marekani ambaye ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na rais mstaafu wa nchi hiyo, Barack Obama.

Emoji ya kicheko yashika nafasi ya kwanza
Emoji imekuwa ni miongoni mwa alama, stika zinazotumiwa na mitandao ya kijamii katika kurahisisha mawasiliano, watumiaji wanapokuwa wanabadilishana mawazo na kuchati mtandaoni.
Katika tathmini ya Twitter kwa mwaka 2019, mtandaoni huo umebaini kuwa emoji ya kicheko ndiyo imeshuka nafasi ya kwanza miongoni mwa emoji 10 ambazo zilitumika zaidi na watumiaji wa Twitter.
Zinazohusiana
- Twitter kuwawekea watumiaji wake muonekano mpya
- Facebook kuzuia matangazo ya ‘uponyaji wa miujiza’ mtandaoni
- Maboresho: Kupitia Twitter utatazama video mubashara
Huenda mwaka huu ulikuwa ni kicheko kwa watu wengi. Lakini emoji ya kilio imeshika nafasi ya pili ikichuana vikali na emoji ya kicheko na kuweka msawazo wa hisia za watu.
Alt Text: 2019 Top emojis worldwide
1. ?
2. ?
3. ?
4. ?
5. ?
6. ?
7. ?
8. ?
9. ❤️
10. ?— Twitter Data (@TwitterData) December 9, 2019
#Hashtag 10 zilizotikisa mwaka huu
Hashatag ya #NotreDame iliyoshika nafasi ya kwanza ilianza kutumika mara baada sehemu ya jengo la kanisa kongwe la Notre Dame la mjini Paris nchini Ufaransa kuteketea kwa moto na kuharibika mapema Aprili mwaka huu.
Jengo hilo la historia lina miaka 850 lilloungua wakati linafanyiwa ukarabati limekuwa alama kuu ya Ufaransa na kivutio kikubwa kwa watalii wanaotembelea nchi hiyo.
Nafasi ya pili imeenda kwa hashatag ya #StartOfReiwaEra, #Venezuela imeshika nafasi ya tatu, #Brexit katika nafasi ya nne.

Hashtag hutumiwa na mitandao ya kijamii kuweka mkazo wa jambo fulani ili kuongeza uwajibikaji na kuibua mjadala kwenye jamii.
Filamu 10 bora
10 bora ya filamu iliyojadiliwa zaidi Twitter mwaka huu inaongozwa na filamu ya “Avengers:Endgame” ambayo imekuwa gumzo kwa wapenda filamu duniani kutokana na visa mbalimbali vinatoa mafunzo lukuki katika maisha.

Orodha hiyo iliyotolewa jana Desemba 10 ni ndefu inahusisha pia vipindi vya televisheni, wachezaji mpira, waigizaji, wanamuziki na timu za mpira ambapo klabu ya FC Barcelona ya Hispania ndiyo iliteka zaidi mijadala ya Twitter.
Orodha hiyo itajitokeza tena mwaka 2020 au itabadilika?