NMB yavipeleka vikundi vya ujasiriamali kidijitali

May 27, 2020 11:04 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Yazindua akaunti mpya ya benki inayofunguliwa kwa simu ya mkononi.
  • Ni maalum kwa ajili ya vikundi vya kijamii na kiuchumi.

Dar es Salaam. Ni dhahiri kuwa ushindani katika sekta ya benki nchini unazidi kuongezeka baada ya benki ya NMB kuzindua akaunti mpya ya benki  inayowawezesha watu waliopo kwenye vikundi kuchangishana na kutunza pesa kwa njia ya simu za mkononi. 

Hudum hiyo iliyopewa jina la “NMB Pamoja Akaunti” ni mahususi kwa wanachama wa vikundi rasmi na visivyo rasmi ambavyo vinajishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo za ujasiriamali. 

Afisa Mkuu wa wateja binafsi, biashara ndogo ndogo na kati wa benki hiyo Filbert Mponzi amesema huduma hiyo inalenga kuwarahisishia Watanzania kupata huduma za kibenki katika viganja vya mikono yao. 

“Ukiwa na NMB Pamoja hautahitajika kwenda katika matawi yetu ili uweze kufungua akaunti ya kikundi,” amesema Mponzi wakati wa uzinduzi huduma hiyo mpya Jumatano (Mei 27, 2020) jijini Dar es Salaam. 

Akaunti hiyo inafunguliwa na viongozi wa vikundi kwa kupitia simu za mkononi na watakuwa na uwezo wa kuongeza idadi ya wanachama watakavyo ili kuona kinachoendelea katika akaunti hiyo. 

“Wanachama wakishaongezwa katika hii akaunti ambayo ni ya kikundi kwa kupitia simu zao wanaweza kuchanga michango, kuhamisha pesa kutoka simu zao na kuingiza katika akaunti yao,” amesema Mponzi.


Zinazohusiana: 


Hata hivyo, huduma hiyo haitawagusa wasiokuwa na vitambulisho vya Taifa. 

Wanachama wenye kitambulisho cha Taifa baada ya kukamilisha taratibu za usajili watakuwa na fursa ya kuanza kuitumia wakati wowote. 

Akaunti hii inatoa urahisi kwa vikundi kugawana pesa na mikopo kwa njia ya simu bila kwenda benki huku ikiwa na uwezo wa kutunza taarifa zote za wanachama na michango yao kwa uwazi. 

Ujio wa kaunti hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa sera jumuishi za kifedha ambazo zinahimiza matumizi ya mifumo ya kidijitali kuziimarisha benki na kuvutia watu wengi kutumia huduma za kifedha kufanya malipo na manunuzi. 

Mwaka 2018, benki hiyo iliingiza sokoni huduma tatu za kibenki kidijitali ikiwemo ya kufungua akaunti ya benki ndani ya dakika tatu kwa kutumia simu ya mkononi ikilenga zaidi kujenga jamii isiyotegemea pesa za mifukoni (Cashless society).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV