Ni uboreshaji wa huduma: Kutoka TiME Tickets hadi Tukiio
- Kampuni hiyo ya kuuza tiketi za matukio yajiboresha.
Dar es Salaam. Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakitumia mtandao kupata tiketi za kuhudhuria matukio mbalimbali basi ‘TiMe Tickets’ siyo jina geni kwako.
Kampuni hiyo imekuja kivingine na sasa inajulikana kama Tukiio, ikiwa ni hatua ya kuboresha shughuli na kuimarisha uhusiano na wateja wake.
Taarifa ya kampuni hiyo iliyotolewa Septemba 20, 2022 imeeleza kuwa “hii ni sehemu ya mageuzi yanayoendelea ya kuboresha bidhaa zetu ili kukidhi uzuri wa kudumu katika urahisi, uwazi na ufanisi.”
“Tukiio inatazamiwa kuwa bidhaa ya kisasa zaidi, thabiti na ya hali ya juu zaidi ambayo tumewahi kuunda – na itabadilisha jinsi matukio yanavyopangwa kote Afrika,” imeeleza taarifa hiyo.
Soma zaidi:
Maboresho yaliyokuja
Huenda hatua hiyo itasaidia zaidi mashirika na biashara mbalimbali kudhibiti matukio ya binafsi na ya umma, uanzishaji, utangazaji/ utiririshaji wa moja kwa moja.
Tukiio pia itakuwa na akaunti maalum za mawakala ili kupanua ujumuishaji wa wadau mbalimbali katika kufanya uzoefu wa matukio kuwa bora zaidi.
Waandaaji wanapotumia Tukiio hivi sasa wanaweza kudhibiti mwenendo wa matukio yao, kama uuzaji wa tiketi na beji, kuwashirikisha waalikwa ajenda, na usajili wa wanaohudhuria popote walipo kupitia programu ya simu.
Kampuni hiyo imeongeza njia za kufanya malipo na sasa watumiaji wanaweza kufanya malipo ya tiketi mtandaoni kwenye zaidi ya benki 13 nchini, kupitia mitandao ya simu pamoja na kadi za mkopo (Credit Card).
Waalikwa wasiotumia mtandao wana nafasi ya kuhakiki tiketi zao kabla ya kuzinunua na wanaruhusiwa kuwapa watu wengine tiketi kuhudhuria mwaliko.
Kwa matukio ya mialiko inayolipiwa kamisheni ya asilimia 7 ya ada ya tiketi itatozwa ili kufidia gharama ya njia za malipo zilizotumika na kushughulikia ada za uhamisho.
Gharama zitakatwa wakati malipo yako ya mfuko yatatumwa kwenye akaunti yako unayotumia. Pesa zote kutokana na mauzo ya tiketi zitachakatwa kwenda kwenye akaunti yako ndani ya saa 24 baada ya ombi.
Latest
