Ndugai kuzikwa Kongwa Agosti 11, 2025

August 8, 2025 11:46 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baaada ya ibada ya kuagwa itakayofanyika katika viwanja vya Bunge Agosti 10, 2025 jijini Dodoma.  

Dar es Salaam. Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatatu, Agosti 11, 2025 nyumbani kwake Kongwa, mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson, wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu jijini Dodoma, shughuli za kumuaga kitaifa zitafanyika siku ya Jumapili, Agosti 10, 2025 asubuhi katika viwanja vya Bunge.

 Tulia amesema siku ya Jumatatu, Agosti 11, mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea nyumbani kwake Kongwa kwa ajili ya kupumzishwa.

Ndugai alifariki dunia Agosti 6, 2025 jijini Dodoma akiwa na umri wa miaka 62. Hata hivyo, chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi na familia pamoja na viongozi wa Bunge.

Ndugai alizaliwa Januari 22, 1963, na alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kongwa kwa miaka kadhaa kabla ya kuchaguliwa kuwa Naibu Spika mwaka 2010.

Baadaye alihudumu kama Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2015 hadi alipojiuzulu Januari 2022.

Hata hivyo, Spika Tulia amesema  marehemu Ndugai alikuwa kiongozi mwenye msimamo imara katika masuala mbalimbali, jambo alilojifunza na kulithamini.

“Ni sehemu ya kiongozi kuwa na msimamo, kwa hiyo nilijifunza kuwa na misimamo na kusimamia jambo,” amesema Dk.Tulia.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV