Namna ya kushughulika na tatizo la kupooza mwili kwa muda mfupi

September 4, 2021 9:55 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni hali ya kushindwa kufanya chochote baada ya kutoka usingizini.
  • Unashauriwa kufanya mazoezi, kuzingatia mlo na kutatua msongo wa mawazo.

Dar es Salaam. Kwa baadhi wanaweza kuelewa ninachotaka kuzungumzia leo. Lakini kwa wengine huenda likawa ni jambo geni.

Baadhi ya siku ambazo nikienda kulala, nalala vyema kabisa. Nitashtuka usiku kunywa maji na nitalala tena hadi kupambazuke. Ni siku za usiku wa kawaida.

Lakini zipo siku ambazo nilikuwa nikishtuka usiku na kujikuta kwenye hali isiyo ya kawaida na kuniacha na mawazo mengi pasipo na majibu.

Nilikuwa nikishtuka usiku na kujikuta siwezi kutikisa hata kiungo kimoja cha mwili wangu. Siwezi kufumbua macho, siwezi kumwita mtu yeyote anisaidie wala kugeuka. Najijua nimeamka lakini siwezi kufanya lolote.

Kuna wakati nilihisi ndiyo nimeaga dunia, namsubiri malaika anionyeshe lango nalopaswa kwenda.

Hata baada ya  hali hiyo kuisha, sikuwahi kutafuta msaada kwani haikuwa changamoto ya mara kwa mara na sikutaka watu waanze kuninyeshea  mvua ya mawazo yao kwani hawakawii kuwahusisha wanga kwenye kila kitu.

Yote yalibadilika siku nilipomsikia mtu mwingine akiongelea hali hiyo. Ni siku hiyo, ndiyo nilijua kuwa changamoto hiyo ina hadi jina, kupooza ukiwa usingini au kitaalamu, “sleep paralysis”.


Kupooza huku ndiyo kukoje?

Licha ya kuwa changamoto hii ni kitu kigeni kwa baadhi lakini watafiti wa masuala ya usingizi wanasema ni ishara ya kuwa mwili wako haupitii hatua zote zinazotakiwa kupitiwa katika usingizi.

Yapo maelezo mengi ya kitaalamu nyuma ya kupooza huku lakini kama wewe siyo mdau wa sayansi huenda ikakuwia ngumu kuelewa. Kwa urahisi ni kuwa, hali hiyo inatokea pale ubongo wako unapoamka kabla ya mwili wako hasa kwenye muda ambao huwa unapata ndoto zako.

Mwandishi kutoka tovuti ya Vital Record, Dominic Hernandez ameweka wazi kuwa, hali hiyo husababishwa kwa makusudi na ubongo wako ili usijikute ukiyafanya yale uliyokuwa ukiyafanya ndotoni.

Fikiria hili, kama unaota unakimbizwa na kitu cha kutisha na uamke ujikute unakimbia kweli. Haitokuwa sawa. Hivyo kupooza ukiwa usingizini kunasaidia usifanye vitendo ambavyo unavifanya ukiwa ndotoni ikiwemo kutembea na kukimbia.

Kwenye hali hiyo, baaadhi huhisi kuwa kuna mtu chumbani kwao, wengine huhisi kukandamizwa na wengine kukabwa. Hata hivyo hayo ni mawazo tu.

Hali hiyoo inaweza kudumu kwa sekunde hadi dakika kadhaa. Picha| The Guardian Nigeria.

Imani nayo imechukua mkondo wake

Mwandishi wa masuala ya afya wa tovuti ya masuala ya afya, WebMd, Beth Roybal ameandika kuwa kwenye baadhi ya jamii, hali hiyo imekuwa ikihusishwa na masuala ya kiimani ikiwemo “mapepo yasiyotaka kuonekana”. Hata hivyo, hayo siyo ukweli.

“Unaweza kuwa kwenye hali hii kwa sekunde na hadi dakika. Kwa baadhi ya watu wanaweza kuhisi presha na kukabwa,” ameandika Roybal akiongeza kuwa hali hiyo inaweza kutokea wakati mtu anaanza kulala, wakati mtu anaamka na hata akiwa usingizini.

Mwandishi huyo ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya afya ameandika kuwa, hali hiyo inawaakuta watu watano kati ya 10 duniani na inasababishwa na tabia mbalimbali ikiwemo kushindwa kupata usingizi, msongo wa mawazo na historia ya familia kuwa na hali hiyo.

Pamoja na hayo, zipo tabia binafsi ambazo huchochea hali hiyo kutokea ikiwemo kulalia mgongo (chali) na kula chakula kingi wakati wa kwenda kulala. 


Tiba ya hali hiyo hii hapa

Watafiti nchini Marekani wanasema hali hii huanza kuwapata watu wenye miaka 14 n akuendela licha ya kuwa hali hiyo inaweza kumtatiza mtu yoyote na haina madhara yoyote. 

“Hakuna uchunguzi wowote wa kiafya unaohitajika,” ameandika Crista O’connell kwenye tovuti ya masuala ya kiafya ya Healthline.

                     

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW