MTN, Airtel yaripoti hasara mitandao ya kijamii ikifunguliwa Uganda
- Ni baada ya takriban siku 13 tangu kufungiwa kwa mitandao ya kijamii kupisha uchaguzi mkuu.
Dar es Salaam. Serikali ya Uganda imefuta marufuku ya mitandao ya kijamii iliyokuwa imewekwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Januari 15, 2026, huku makampuni makubwa ya mtandao yakiripoti hasara ya Sh17.8 bilioni.
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba katika taarifa yake iliyochapishwa jana Januari 26, 2026 katika mtandao wa X amewashukuru wananchi wa Uganda kwa kushirikiana vyema katika kipindi chote cha marufuku hiyo.
“Tunafungua mitandao yote ya kijamii leo… Mungu awabariki wote,” amechapicha Muhoozi katika jukwaa la X.
Kufunguliwa kwa mitandao ya kijamii nchini humo kunakuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu kuanza kwa marufuku hiyo Januari 13, 2026, siku mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Januari 15, 2026.

Mbali na tukio hilo, kukosolewa vikali na wapinzani wa kisiasa na mashirika ya haki za kiraia, mamlaka za mawasiliano nchini humo zilisema hatua hiyo ililenga kulinda usalama wa Taifa, kuzuia habari zisizo sahihi na kuzuia vurugu za kisiasa
Ingawa huduma ya intaneti kwa ujumla ilianza kurejeshwa kidogo kidogo kuanzia Januari 17 mwaka huu, bado wananchi walilazimika kutumia VPN ili kupata huduma za muhimu na kufanya miamala ya kidigitali hatua ilioyopoteza mapato ya Sh 17.8 bilioni kwa kampuni kubwa za mawasiliano ikiwemo MTN na Airtel.
Kwa sasa, wananchi wa Uganda wanaweza kutumia mitandao ya kijamii bila VPN, jambo linaloashiria kurejea kwa hali ya kawaida ya shughuli za kidijitali.
Hata hivyo, baadhi ya majukwaa kama Facebook bado yanaripotiwa kuwa na vizuizi vidogo au kutokuwa na ufikiaji bila VPN.
Latest