Msako wanaomiliki silaha isivyo halali kuanza kesho

November 30, 2021 2:46 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Baada ya tarehe ya mwisho kusalimisha silaha hizo kuisha leo.
  • Watakaokutwa nazo kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Mwanza. Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limesema kuanzia kesho litaanza msako wa silaha zinazomilikiwa isivyo halali huku likipokea silaha tano zilizosalimishwa na watu katika vituo vya polisi.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ramadhani Ng’anzi amesema kati ya silaha hizo tatu ni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, moja wilayani Magu na iliyobaki imesalimishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.

Kusalimishwa kwa silaha hizo kunatokana na agizo la Serikali la hivi karibuni la kuwataka watu wote wanaomiliki silaha isivyo halali kuziwasilishwa katika vituo vya polisi au ofisi wa watendaji kata kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.

“Waziri (wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene) alitoa tangazo hilo mwezi mmoja uliopita kuwa wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wazisalimishe kwenye ofisi na vituo mbalimbali vya serikali vilivyokaribu nao kabla msako haujaanza kufanyika, tunashukru wananchi wamejitokeza na Mwanza tumepokea silaha tano,” amesema Kamanda Ng’anzi

Kamanda huyo amesema bado wanaendelea kupokea silaha hizo hadi leo saa 6 usiku, hivyo wananchi wote ambao wanamiliki silaha kinyume cha sheria ofisi za serikali ziko wazi.

“Nitoe wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza ambao wanazimiliki isivyo halali wasalimishe katika vituo vya polisi, watendaji kata, watu wa serikali za mitaa. Wasipofanya hivyo hatua kali,” amesema kamanda huyo.

Amesema kuanzia kesho watapita nyumba kwa nyumba kuzisaka silaha zote ambavyo zinamilikiwa isivyo halali na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokamatwa nazo. 

Silaha hizo ambazo hazimilikiwi isivyo halali zimekuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo ujambazaji, unyang’anyi na hivyo kusababisha hasara kwa watu za mali na hata vifo. 

Vitendo hivyo, uiongezea Serikali kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zake. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
12 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV