Morogoro inavyokimbiza uzalishaji wa nyanya

March 18, 2020 2:42 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya kulima zaidi ya nusu ya nyanya zote Tanzania bara.
  • Morogoro imefuatiwa na mkoa wa Kilimanjaro na Mtwara.
  • Mkoa huo ulizalisha tani 155,745 sawa na asilimia 65.5 ya nyanya zote zilizozalishwa mwaka huo.

Dar es Salaam. Mkoa wa Morogoro umetajwa kuongoza kwa kilimo cha nyanya baada ya kuzalisha zaidi ya nusu ya nyanya zote Tanzania bara. 

Kwa mujibu wa ripoti ya Utafiti wa Mwaka wa Sekta ya Kilimo (AAS 2016/2017) iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mwaka 2016/2017 mkoa huo ulizalisha tani 155,745 sawa na asilimia 65.5 ya nyanya zote zilizozalishwa mwaka huo. 

Hiyo ni sawa na kusema zaidi ya nusu ya nyanya zote zinazozalishwa Tanzania zinatoka katika mkoa huo unaopatikana Mashariki mwaka Tanzania. 

Morogoro inafuatiwa kwa mbali na Kilimanjaro ambayo iliyozalisha tani 18,630 na Mtwara katika nafasi ya tatu baada ya kuzalisha tani 13,336.

Nyanya limekuwa ni zao la mboga ambalo linatumiwa zaidi katika shughuli za mapishi nyumbani na usindikaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo nyanya za kopo. 

Habari hii imeboreshwa kiunganishi (link) ya chanzo cha takwimu Machi 8, 2020.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
NISHATI

NISHATI

Nukta TV

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Nukta TV

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Nukta TV