Milana: Vita ya Ukraine imenitengisha na baba yangu

March 16, 2022 7:08 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni mtoto katika moja ya familia ambaye ni mkimbizi nchini Ukraine.
  • Baba yake Yevgenii yuko vitani dhidi ya majeshi ya Urusi.
  •  Ana matumaini siku moja atakutana tena na baba yake.

Dar es Salaam. Ni siku 22 sasa tangu Urusi ianzishe mashambulizi yake nchini Ukraine, kitendo ambacho  kimetenganisha familia na kuleta upweke katika familia.

Hiyo ni baada ya wanaume kubaki Ukraine ili kupigana vitani huku familia zao zikilazimika kukimbilia maeneo mengine ya taifa hilo na hata nje ya Ukraine.

Kwa mujibu wa kituo cha mawasiliano cha Umoja wa Mataifa, miongoni mwa familia zilizoathirika ni ya Yevgenii na mkewe Oleksandra ambao wana watoto wawili wa kike Milana na Polina.

Mashambulizi yalipoanza Februari 24, 2022, familia hiyo ililazimika kuondoka kwenye makazi yake jimboni Donetsk na kukimbilia jimbo la Zakarppatia lililoko Magharibi mwa Ukraine.

Familia hiyo ilipata  hifadhi katika Chuo Kikuu cha Mukachevo.

Hata hivyo, baba wa familia hiyo alirudi vitani kama Serikali ya Ukraine ilivyoagiza kwa wanaume walio na umri wa mika 18 hadi 60 kubaki nchini na kupambana dhidi ya majeshi ya Urusi. 

“Mume wangu alirudi nyumbani baada ya kutufikisha hapa salama. Serikali inataka wanaume wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 60 wabakie Ukraine waingie jeshini kupambana kukomboa nchi,” amesema Oleksandra wakati akihojiwa na UN.

Kurudi kwa Yevgenii kwenye mapigano kumeleta hofu kwa familia hiyo, kwani hawajui baba huyo wa familia anaendeleaje huko aliko.

Milana (6) ana matumaini kuwa iko siku atamuona baba yake.

“Nitakaporejea, nitaenda kumtembelea bibi yangu. Nina bibi wawili na pia nina babu na baba yangu Yevgenii,” amesema Milana ambaye amechora picha ya baba yake kwenye ukuta wa chumba walichopewa hifadhi.

Pamoja na mashambulizi yanayoendelea Ukraine, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) linashirikiana na mamlaka za mijii ili kupanua huduma za kupokea wakimbizi, sambamba na kubainisha majengo ya kukarabatiwa ili yatumike kama malazi kwa wakimbizi wa ndani.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV