Microsoft mbioni kuingiza sokoni “simu ya Android”

October 3, 2019 7:59 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Inakusudia kuingiza sokoni kifaa kinachofanana na simu janja cha ‘Microsoft Surface duo’ ifikapo 2020.
  • Moja ya sifa yake ya pekee ni uwezo wake wa kutumia mfumo endeshi wa Android ambao hautumiki na simu za Microsoft.

Kampuni ya Microsoft ya nchini Marekani inakusudia kuingiza sokoni kifaa kinachofanana na simu janja cha ‘Microsoft Surface duo’ ifikapo 2020 ili kuwapatia wateja wake bidhaa tofauti na walizozizoea.  

Kampuni hiyo ya kompyuta na vifaa vya kielektroniki imeeleza kuwa kifaa hicho kinachofanana na simu kitakuwa kinaendeshwa na mfumo endeshi wa Android ambao haujazoeleka na watumiaji wa bidhaa za kampuni hiyo. 

Huenda hatua hiyo, ikawapa uchaguzi watumiaji wa simu za Microsoft zinazotumia mfumo wa Windows, kutumia vifaa vyenye muonekano tofauti. 

Kifaa hicho, kina sehemu mbili ya kioo zinazoweza kukunjwa katika muonekano tofauti, zitamuwezesha mtumiaji kupiga simu, kupiga picha kwa kamera na kufanya mambo mengine kama siku za kawaida.

Mkurugenzi Mtendaji wa Microsoft, Satya Nadella amesema kampuni yake inajaribu kutengeneza bidhaa mpya tofauti na zilizozoeleka na kuongeza kuwa hiyo inaweza isiwe simu bali kitu kingine.

Lakini wadadisi wa mambo wanasema, inaweza kuwa ni simu lakini Microsoft haitaki kuweka wazi jambo hilo. Kifaa hicho kinatarajiwa kuingia sokoni na kuanza kutumika mwaka 2020. 


Zinazohusiana:


Mabadiliko huenda yakaleta manufaa makubwa kwa watumiaji wa Microsoft kwani wataweza kupata programu tumishi ambazo hazipatikani kwenye mfumo wa simu za Windows.

Pia inaweza kuifaidisha kampuni hiyo kujitanua kimasoko ili kuwafikia wateja wengi duniani kwa bidhaa bora zinazotumiwa na watu wengi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV