Mfahamu panya wa Tanzania mtegua mabomu aliyefariki dunia

January 14, 2022 2:16 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Septemba 2021, shirika la usaidizi la mifugo la Uingereza (PDSA) lilimtunuku Magawa medali yake ya dhahabu kwa “kujitolea kuokoa maisha katika eneo na uondoaji wa mabomu hatari ya ardhini nchini Cambodia.” Picha| PDSA.


  • Ni panya Magawa mwenye asili ya Tanzania aliyefariki mwishoni mwa wiki.
  • Alikuwa akisifika kwa umahiri wake wa kugundua na kutegua mabomu na vilipuzi nchini Cambondia.
  • Amesaidia kuokoa maelfu ya maisha ya watu. 

Dar es Salaam. Panya mwenye asili ya Tanzania aitwaye Magawa aliyetumika kutafuta na kutegua mabomu ya ardhini na vilipuzi nchini Cambodia amefariki dunia mwishoni mwa wiki akiwa na umri wa miaka nane huku akikumbukwa kwa ushujaa wake  wa kuokoa maisha ya watu yaliyokuwa hatarini.

Shirika la APOPO la nchini Ubelgiji lililokuwa linamlea Magawa katika taarifa yake iliyotolewa leo katika ukurasa wake wa Instagram limesema panya huyo ameaga dunia akiwa na miaka nane mwishoni mwa wiki.

“Ni kwa moyo wa masikitiko kwamba tunatoa taarifa za kusikitisha kwamba shujaa Magawa aliaga dunia kwa amani wikendi hii,” imeeleza taarifa ya APOPO. 

Kwa mujibu wa APOPO, shirika linalotoa mafunzo kwa wanyama ya kuokoa maisha ya watu, Magawa alikuwa na afya nzuri na alitumia muda mwingi wa wiki iliyopita kucheza kwa shauku yake ya kawaida.

Hata hivyo, kuelekea mwishoni mwa wiki alianza kupunguza kasi, kulala zaidi na kuonyesha hamu kidogo ya chakula katika siku zake za mwisho. 

Magawa aliyesheherehekea siku yake ya kuzaliwa Novemba 2021 amefika tamati ya maisha katika umri wa uzee wa miaka nane.

Shirika hilo limesema limeguswa na kifo cha panya huyo shujaa na kushukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya siku za uhai wake. 

Wakati wa kazi yake, Magawa alipata zaidi ya mabomu 100 ya ardhini na vilipuzi vingine, na kumfanya kuwa shujaa wa APOPO aliyefanikiwa zaidi hadi sasa. 

Mchango wake umesaidia  watu nchini Cambodia kuishi, kufanya kazi na kucheza bila hofu ya kupoteza maisha au viungo vya mwili kutokana na mabaki ya vilipuzi vya migodini na mabomu baada ya kumalizika kwa vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe miaka ya 1970 na 1980.


Soma zaidi:


Ushujaa wa kutegua mabomu

Magawa alistaafu Juni mwaka 2021 baada ya kuhitimisha kazi yake ya miaka mingi ya kugundua mabomu ya ardhini nchini Cambodia. 

Magawa, aliyekuwa na asili ya Tanzania, amekuwa panya aliyefanikiwa zaidi kufunzwa na kusimamiwa na APOPO kunusa mabomu ya ardhini na kutoa tahadhari kwa wachimbaji ili waweze kuondoa vilipuzi kwa usalama.

Kwa mujibu wa APOPO, Magawa alisaidia kuondoa migodi kutoka eneo la mita za mraba 225,000 (futi za mraba milioni 2.4).

Kifo cha Magawa huenda siyo cha bahati mbaya kwa sababu kwa wastani wa maisha ya panya mkubwa wa Kiafrika ni miaka nane.

Panya Magawa akiwa katika mafunzo ya kutegua mabomu kabla hajafariki dunia. Picha| PDSA UK.

Panya aliyeshinda tuzo

Septemba 2021, shirika la usaidizi la mifugo la Uingereza (PDSA) lilimtunuku Magawa medali yake ya dhahabu kwa “kujitolea kuokoa maisha katika eneo na uondoaji wa mabomu hatari ya ardhini nchini Cambodia.”

Ndiye panya wa kwanza kuwahi kushinda tuzo ya ushujaa na heshima ambayo hapo awali ilikuwa imetengwa kwa ajili ya mbwa pekee.

Ukubwa wa panya wa Kiafrika waliofugwa huwawezesha kutembea katika maeneo ya migodi bila kufyatua vilipuzi na kwa kasi zaidi kuliko binadamu aliye na kigunduzi cha chuma.

Mwaka jana, APOPO ilifanikiwa kuwafunza panya 20 na kuwapeleka Cambodia ili kuendeleza kazi ya kugundua vilipuza katika maeneo yaliyokuwa na migodi.

Kwa mujibu wa Kituo cha Utekelezaji cha Migodi ya Cambodia (CMAC), bado kuna mabaki takriban milioni 6 ya vilipuzi ambavyo viko ardhini vinavyotakiwa kuteguliwa. 

Panya wa Tanzania wamekuwa maarufu duniani hasa katika shughuli za kugundua na kutegua mabomu ikiwemo nchini Msumbiji.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV