Mengi awasili Kilimanjaro, Majaliwa kuongoza mazishi yake kesho

May 8, 2019 11:37 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Familia ya Mengi wakiwemo watoto wake wakimsindikiza mpendwa wao katika safari yake ya mwisho duniani. Picha|Mtandao


  • Tayari mwili wa mfanyabiashara huyo umewasili mkoani Kilimanjaro na kupokelewa na wakazi wa mkoa huo ambapo mazishi yatafanyika kesho kijijini kwake Nkuu, Machame. 

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza mazishi ya Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi yatakayofanyika kesho Mei 9, 2019 Machame, wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Majaliwa ataongoza mazishi hayo kwa niaba ya Serikali ambapo ibada ya mazishi itafanyika katika  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Kisereni, Machame na baadaye atazikwa katika makaburi ya familia.

Mwili wa marehemu Mengi tayari umewasili mkoani Kilimanjaro ukitokea jiji la Dar es Salaam ambapo ulipokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shirika la ndege la  Precision Air .

Baada ya kuwasili, msafara wa magari yaliyowabeba waombolezaji na mwili wa marehemu umeelekea Machame kwa ajili ya taratibu za mazishi. 

Mapokezi ya Mengi katika uwanja wa KIA yaliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira na viongozi wengine wa Serikali wakiwemo wakuu wa wilaya na viongozi wa kijamii. 

Mengi alifariki dunia mjini Dubai, Falme za Kiarabu usiku wa kumkia Mei 2, 2019 na mwili wake uliwasili Mei 6 ambapo jana mfanyabiashara huyo alipewa heshima za mwisho katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. 


Soma zaidi:


Jana Mei 7, Rais John Magufuli aliwaongoza wakazi wa jiji hilo kumuaga Mengi huku watu waliokuwepo katika eneo hilo wakimuelezea kwa namna tofauti hasa mchango wake aliouacha katika ujenzi wa uchumi wa nchi kwa kutoa nafasi za ajira kwa watu mbalimbali.

Mamia ya wakazi wa Machame wamejitokeza kumpokea mpendwa wao, kuonyesha jinsi alivyoacha alama katika mioyo yao.

 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV