Mbaroni kwa kuuza jezi feki za Yanga, Simba

July 13, 2022 11:32 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni Said Furaha akutwa na jezi feki dazani 296.
  • Atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Mwanza. Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikiria Said Furaha (31) kwa tuhuma za kukutwa na jezi feki za timu za Simba na Yanga dazani 296.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng’anzi aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 13, 2022 amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Julai 5 mwaka huu katika eneo la Pamba road Sokoi Wilaya ya Nyamagana.

Amesema kuwa kati ya jezi hizo dazani 145 ni za nembo ya klabu ya Simba na dazani 151 ni za kablu ya Yanga inayofadhiliwa na kampuni ya GSM.

Kamanda Ng’anzi amesema walipata  taarifa toka kwa afisa masoko wa kampuni ya GSM na Vunja bei kuwepo kwa mfanyabiashara anayesambaza na kuuza jezi hizo bandia.

“Baada ya taarifa hizo ufuatiliaji wa kina na haraka ulifanyika na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa tajwa hapo juu akiwa na jezi hizo bandia za klabu ya Simba na Yanga dukani kwake,” amesema  Kamanda Ng’anzi.

Amesema polisi wanaendelea kufanya upelelezi wa kina kuhusiana na shauri hilo ili kuweza kubaini mtandao mzima wa wahusika wote wanaotengeneza, kuagiza na kuingiza nchini bidhaa hizo bandia suala linachongangia wadhamini wa klabu hizo kukosa mapato.

“Upelelezi wa shauri hili unakamilishwa mara moja na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo,” amesisitiza kamanda huyo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV