Mapato yasiyokusanywa Serikali za mitaa yaongezeka kwa asilimia 61.7

November 2, 2023 3:13 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ongezeko hilo linatokana na uzembe wa wakurugenzi katika usimamizi wa mapato ya halmashauri.
  • Kamati yapendekeza kuchukuliwa hatua na kurejeshwa kwa mapato ya Serikali yaliyopotea.

Dar es Salaam. Huenda Serikali ikakabiliwa na upungufu wa mapato kutoka serikali za mitaa jambo litalosababisha kukwama kwa shughuli za maendeleo na kupeleka maumivu kwa wananchi kutokana na uzembe wa kutokusanya kwa mapato hayo.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) imebaini kunanongezeko la asilimia 61.7 la kutokukusanya mapato ya Serikali za mitaa jambo linaloongeza mzigo wa gharama kwa Serikali kuu.

Kwa mujibu wa LAAC mapato yasiyokusanywa yameongezeka kutoka Sh12.49 bilioni iliyorekodiwa mwaka 2020/2021 hadi Sh37.33 billioni  mwaka 2021/2022 katika halmashauri 146 nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa LAAC Halima Mdee, aliyekuwa akiwasilisha bungeni taarifa yake iliyochambua ripoti ya ukaguzi wa mamlaka za serikali za mitaa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 leo Novemba 11, 2023, amewaambia wabunge kuwa ongezeko hilo limetokana na  uzembe wa baadhi ya viongozi wa halmashauri.

“Hali hii inatokana na uzembe wa wakurugenzi katika usimamizi wa mapato ya halmashauri,” amesema Mdee jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa ripoti ya CAG, vyanzo visivyokusanywa ni pamoja na  kodi zitokanazo na upangishaji wa maduka na nyumba vilivyopo katika vituo vya mabasi na masoko na kodi za kupangisha vibanda na vizimba vya masoko.

Vyanzo vingine visivyokusanywa mapato ni pamoja na kodi ya nyumba, kodi za upangishaji wa maeneo ya wazi, fukwe, uuzaji wa viwanja, ada za uwindaji,  leseni za biashara, na leseni za vileo.

Endapo fedha hizo zingekusanywa zingeiwezesha Serikali kufanya shughuli mbalimbali ambazo zinahitaji fedha kwa sasa ikiwemo mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa, usambazaji wa huduma za umeme, maji pamoja na huduma za afya.

Katika bajeti ya mwaka huu wa fedha 2023/24 ambapo Serikali imedhamiria kukusanya na kutumia Sh44.39 trilioni, Serikali za Mitaa zimepangiwa kukusanya Sh4.66 trilioni kati ya Sh31.38 zinazotarajiwa kutoka kwenye mapato.


Soma zaidi:‘Betting’, vinywaji baridi kuchangia bima ya afya kwa wote Tanzania


Aidha, kamati hiyo pia imebaini uzembe unaofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) uliochangia kupotea kwa fedha za Serikali ikiwemo Sh11.07 billioni katika halmashauri 98.

Fedha hizo ni zile zilizokusanywa kwa mashine za kukusanya mapato (Pos) na kutakiwa kuwasilishwa benki lakini badala yake viongozi wa maeneo husika walizitumia katika matumizi mengine.

“Wakurugenzi wamekuwa kutumia Takukuru kama kichaka cha kutochukua hatua dhidi ya wakusanya mapato ambao wamekuwa wakijichukulia fedha na kutumia kwa matumizi mengine baada ya kuziwasilisha benki,” ameongeza Mdee.

Muarobaini wapendekezwa

Kamati hiyo imeishauri  Serikali kuhakikisha fedha zote zilizokusanywa kupita mashine za Pos zinawasilishwa benki kabla ya mwezi Aprili 2023 pamoja na kukusanywa kwa fedha katika vyanzo vyote muhimu vya mapato ya ndani.

Serikali za mitaa kupitia Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 sura 290  zimepewa mamlaka ya kukusanya mapato katika maeneo mbalimbali ikiwemo masoko, vituo vya mabasi, kodi za mapango, na leseni za uuzaji vileo.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
21 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV

NMB BANK YATANGAZA GAWIO LA SH610 KWA HISA 2025

NMB BANK YATANGAZA GAWIO LA SH610 KWA HISA 2025

Nukta TV

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV