Mapato ya madini yazidi kumpa tabasamu Rais Magufuli

July 25, 2019 8:50 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Katika miaka yote miwili iliyopita Serikali ilivuka lengo la ukusanyaji mapato kutoka katika sekta ya madini. 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli hapana shaka sasa ameanza kupata tabasamu baada ya mapato yatonayo na sekta ya madini kupaa ndani ya miaka miwili huku yakizidi malengo ya ukusanyaji.

Jana katika hafla ya kupokea kilo 34 za dhahabu zilizokamatwa kutoka nchini Kenya, Dk Magufuli alieleza kuwa jitihada za udhibiti wa sekta hiyo ikiwemo utoroshwaji wa madini zimesaidia kuongeza mapato ya Serikali kutoka katika sekta hiyo.

Kwa data za mapato alizozitoa Rais Magufuli jana (Julai 24, 2019), mapato kutoka katika sekta hiyo yameongezeka zaidi ya mara na nusu ya lengo la mwaka 2017/18 huku Serikali ikitarajia kuingiza kiasi kikubwa zaidi katika mwaka wa fedha wa 2019/20 ulioanza mwezi huu.

Kuongezeka kwa mapato hayo kunazidi kuisaidia Serikali ya Rais Magufuli ambayo inaendelea kufanya uwezekezaji mkubwa wa miundombinu ya maendeleo inayogharimu matrilioni ya Shilingi ikiwemo reli ya kisasa (SGR) na ujenzi wa mradi wa maporomoko ya maji ya Rufiji.

Mapato ya Sh335 bilioni yaliyopatikana katika sekta ya madini mwaka 2018/19 yanatosha kuihudumia bajeti nzima ya Wizara ya Kilimo ya 253.85 bilioni ya mwaka 2019/20 na chenji juu ili kusaidia kunyanyua maisha ya wakulima nchini. 

Nyumbua zaidi data hizo hapa chini.

Enable Notifications OK No thanks