Mambo ya kuzingatia unapoipanga sebule yako

April 28, 2020 9:40 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Hakikisha vitu na urembo unaoweka unaendana na ukubwa sebule yako. 
  • Paka rangi angavu inayovutia na yenye mwonekano mzuri. 
  • Kama bajeti haitoshi, weka vitu vya msingi na mengine yatafuata baadaye.

Dar es Salaam. “Niweke nini katika sebule yangu” huenda ni swali ambalo kila mwenye nyumba hujiuliza mara baada ya kuhamia kwenye nyumba mpya.

Hata hivyo, mawazo hayo huweza kuwa rahisi endapo utazingatia vitu vichache vitakavyofanya upangaji wa sebule yako kuwa rahisi na kuepukana na majuto hapo mbeleni endapo mambo yataenda kombo yakiwemo kuvunjika kwa vitu. 

Hivi ni baadhi ya vitu muhimu kufahamu

  1. Ukubwa wa sebule yako

Sebule kubwa itakupatia nafasi ya kuweka vitu vingi ili isionekana kuwa tupu. Ni vizuri vitu hivyo pia vikaendana na ukubwa wa sebule yako.

Jarida la Forbes limependekeza kutumia vyungu vya mapambo vikubwa na mimea ambayo haina ushindani wa hewa ya oksijeni wakati wa usiku.

Kutumia vyungu, michoro ya ukutani itakuwa kitu cha kuanzia unapowaza juu ya kupamba sebule yako.

Kama sebule yako ni ndogo, hauna haja ya kuijaza vitu vingi kwani utakosa hata mzunguko wa hewa kwenye sebule yako.

Kama sebule yako ni ndogo, hauna haja ya kuijaza vitu vingi. Picha| Giphy.

  1. Rangi iliyopakwa kwenye sebule yako

Ukilizingatia hili pia, hauna ulazima wa kuwa na mawazo sana kwani hicho pia ni kitu kimojawapo cha kuangalia.

Kwa kuangalia rangi yako, itakupa urahisi wa pazia unazotakiwa kuweka, makochi yatakayorandana nayo na mapambo ya sebuleni. Hakuna mtu anayefurahia rangi kachumbari kwenye sebule yake.

Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya mwanga wanashauri kupaka rangi angavu sebuleni ili mwanga uweze kutosha.

  1. Wanafamilia wako

Ni hakika kuwa unawafahamu wanafamilia wako na uwezo wao wa kujali vitu. Kama ndiyo hivyo, ni dhahiri kuwa utanunua mapambo na vitu vinavyohitaji umakini mkubwa na kuviweka kwenye sebule yako.

Monica Meshack ambaye ni mama wa watoto watatu, mkazi wa Mkoa wa Shinyanga amesema watoto wake ni watundu sana na hivyo wamepasua vitu vingi sebuleni kwake vikiwemo vyungu vya mapambo na vitu vingine vingi. 

Hilo limemfundisha kuwa makini pale anapohitaji kuipendezesha sebule yake tena.


Zinazohusiana


  1. Bajeti yako na mapendeleo

Hauna haja ya kutafuta makubwa wakati mfuko wako hauruhusu. Unaweza kutafuta samani za nyumbani kwako ambazo zipo kwenye bajeti yako na bado sebule yako ikaonekana vizuri.

Hata hivyo, hauna haraka kwani kujaza sebule yako siyo sifa. Ni muhimu kuangazia vitu vya muhimu viwepo na mengine yatafuata.

Grace Mzee mkazi wa Segerea jijini Dar es Salaam amesema vitu kama makochi, televisheni, na meza za sebuleni ni muhimu kuanzia na mambo mengine yanaweza kufuatia.

“Sebule haiwezi kukosa sehemu ya kukaa na meza kwa ajili ya kuhudumia wageni vinywaji n.k. Hamna haraka, nunua vya muhimu kwanza,” amesema Mzee.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV